BANDA MEDIA BLOG

MAKAMPUNI 100 YA NCHINI CHINA KUTUA NCHINI MACHI MWAKA HUU ILI KUONA UWEZEKANO WA KUWEKEZA KATIKA VIWANDA


Nashukuru kupata fursa ya kukutana na Bi. Wenhui Tian Naibu Mkurugenzi (Deputy Director) wa "China Africa Fund For Poverty Reduction and Development" ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa "China-Asia Economic Development Association Overseas Cooperation committee" aliyeambatana na naibu katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Bw. Alex Liu
Kwa pamoja nikiwa na ndugu yangu Gavana Michael Semindu, tofauti na kufahamiana na Viongozi hawa muhimu katika taasisi hizi kubwa nchini China, tuliweza kufahamu namna wanavyofanya kazi mbalimbali za maendeleo ya Kiuchumi barani Afrika.


Akiongea mmoja wa wanafunzi wanaosoma nchini humo Remidius Mwema Emmanue amesema Tanzania ni miongoni mwa mataifa ambayo yameendelea kufanya kazi na Jumuiya hiyo ambayo imekuwa ikifanya shughuli za uwekezaji barani Afrika kupitia makampuni ya kibiashara kutoka China yenye lengo la kufanya uwekezaji kupitia sekta mbalimbali za kiuchumi ambapo amesema huu nimwendelezo wa Mpango wa China wa kuhamishia Viwanda vyao nje ya China.

 
Remi amekumbusha kuwa Novemba 23, mwaka uliopita Ubalozi wa Tanzania nchini China kwa Kushirikiana na jumuiya hii ya maendeleo ya Kiuchumi uliandaa mkutano mahususi  Beijing China ukilenga kuvutia uwekezaji wa viwanda nchini Tanzania, ambapo wawekezaji Zaidi ya Makampuni hayo 100 kutoka majimbo mbalimbali nchini humo  walishiriki  wakikutana na viongozi waandamizi kutoka Tanzania wakiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na kuonyesha nia ya kuwekeza nchini.
 
aliongeza kuwa hatua inayofuata sasa ni wawekezaji hao kuja Tanzania mapema mwezi Machi mwaka huu, ikiwa ni mwendelezo wa hatua za kufanikisha adhma hiyo ambayo kwa hakika inalenga kuvutia uwekezaji wa Viwanda.
Hatua hizi zimekuwa ni juhudi kubwa za Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa kairuki hususani kipindi hiki ambapo taifa letu limeendelea kutekeleza sera ya Uchumi wa Viwanda kuelekea Uchumi wa kati ifikapo 2025.
 
Tofauti na Tanzania, baadhi tu ya Mataifa mengine ambayo yameendelea kufanya kazi na Jumuiya hii (China-Asia Economic Development Association Overseas Cooperation committee) ni pamoja na Benin, Ivory Coast, Gambia, Uganda,Nigeria ,Ghana,Togo,Angola n.k ambapo kusudio la uwekezaji wa miradi hii mikubwa ya kiuchumi barani Afrika imekuwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa China na Afrika.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG