Watu wawili wamefariki dunia huku wengine
wawiliwakihofiwa kufa maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha juzi Mkoani
Dodoma.

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,Gilles Muroto,alisema waliofariki ni Ramadhan Haruna (46) ambaye alifia katika mashimo ya machimbo ya Nzuguni Manispaa ya Dodoma.
Alimtaja mwingine aliyefariki ni Daudi Luwinga (16) Mkazi wa Nzuguni Manispaa ya Dodoma ambaye alidumbukia katika shimo la choo katika mtaa wa Nzunguni Manispaa ya Dodoma wakati akitoka kuangalia mpira.
Pia Kamanda Muroto alisema watu wawili hawajulikani waliko baada ya kusombwa na maji wakiwa kwenye gari katika eneo la Kikombo Manispaa ya Dodoma.
"Hatujaweza kuwajua majina yao na bado tunaendelea kuwatafuta,"alisema
Aidha Kamanda Muroto akizungumza katika eneo la tukio alitoa onyo kwa mtu yeyote ambaye ataendelea kufanya shughuli zozote za uchimbaji katika mashimo hayo Jeshi la Polisi litamshughulikia.
“Mimi nitakuja na nguvu yangu ya jeshi la polisi na tutakaemkuta hatua kali za kisheria zitachukuliwa hivyo basi nawaombeni wanachi hakuna shughuli yoyote ambayo itaenda kufanyika tena kuanzia sasa, tayari tulisha lipa fidia kwa wakazi wa eneo hili siku nyingi”alisema Kamanda Muroto.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Binilith Mahenge amefunga na kupiga marufuku shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu zilizokuwa zinafanyika katika eneo la machimbo Nzuguni Manispaa ya Dodoma.
Pia Dk. Mahenge ameuagiza UYongozi wa Madini kanda ya kati kwa kushirikiana na uongozi wa Manispaa chini ya Jeshi la polisi kufukia mashimo yote ambayo yalikuwa yanatumika kwajili ya uchimbaji wa madini hayo.
Dk. Mahenge aliitoa marufuku hiyo jana wakati alipokwenda kutembelea machimbo hayo ambapo alisema mtu yoyote atakaekaidi hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
“Naagiza mashimo yote haya yafukiwa aje hapa kamishina wa madini pamoja na uongozi wa Manispaa wayafukie yote na mimi nitakuja kukagua haraka iwezekanavyo,”alisema Dk. Mahenge.
Aidha alisema kuwa machimbo hayo pamoja na kuwa wananchi walikuwa wakiendelea na shughuri za uchimbaji lakini tayari Kamishna wa madini kanda ya kati alishayafungia na barua hizo zipo katika ngazi mbalimbali za serikali mkoani na wilayani.
“Eneo hili tayari lilishafungiwa kwajili ya shughuri za uchimbaji wa madini na kamishina wa madini, kwa kukosa sifa kwani tayari lilishachukuliwa na jeshi la polisi kwajili ya ujenzi wa chuo lakini pia lipo jirani na kambi ya jeshi la wananchi Ihumwa na sio salama kabisa kwajili ya shughuri za uchimbaji madini”alisema Dk. Mahenge.
Naye Meneja wa wakala wa barabara nchini (Tanroad) mkoa wa Dodoma Mhandisi Leonard Chimagu, alisema madaraja matatu yalimeharibiwa vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha kukata mawasiliano ya barabara kukatika.
“Mpaka hivi sasa jumla ya madaraja matatu yameharibiwa na mvua Kikombo mawili na hombolo moja niwaombe wanachi wachukue tahadhari hasa katika kipindi hichi cha mvua kwani madaraja mengi yameharibika,”alisema Mhandisi Chimagu.

Tags
mvua kubwa