Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha
Mwakisebe kata ya Kimaha wilayani chemba mkoani Dodoma amefariki dunia,
huku watu wengine zaidi ya 2000 wakiwa hawana mahali pa kuishi baada ya
nyumba zao kubomoka na nyingine kuzingirwa na maji, kufuatia mvua kubwa
zinazoendelea kunyesha wilayani humo.
Wilaya ya Chemba ni miongoni mwa wilaya mpya zinazopatikana makao makuu ya nchi Dodoma ambapo katika msimu wa mvua hizi za masika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dodoma yamekuwa yakipata mvua nyingi zinazosababisha mafuriko na adhari mbalimbali kujitokeza ikiwemo kuharibika kwa miundombinu ya barabara.
Athari za mvua hizo ambazo zimejitokeza katika vijiji vya Olboloti,Kaloleni na Mrijo Chini ambavyo ndivyo vinavyodaiwa kuwa ndio vimeathiriwa zaidi na mafuriko hayo shughuli za uokozi zikiendelea huku wananchi wakieleza namna walivyoathirika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha OlbolotiAbdalah Suti amesema kuwa mvua iliyonyesha katika maeneo yao ni kubwa na kwamba haijawahi kutokea tangu miaka ya 1960
Amiry Issa ni mkuu wa zimamoto kituo cha Dodoma amesema kuwa kikosi kinaendelea na shughuli za uokozi kuzunguka vijiji hivyo huku akiwataka wananchi kutosogelea maeneo hatarishi.
Mkuu wa wilaya ya Chemba ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya hiyo, Simon Odunga amesema kuwa eneo wanaloishi wananchi hao ni eneo hatarishi kwani wanazungukwa na milima huku akiwataka wananchi waaliojenga katika maeneo ya mabondeni kuhama mara moja
Shughuli za uokozi zilikuwa zikiendelea kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo kikosi cha zimamoto na uokoaji huku baadhi ya wananchi wakionekana kuhamisha vitu vyao
wakati huo huo mvua zilizonyesha usiku kucha wa kuamkia jan 11, mwaka huu zilisababisha hasara ya mimea iliyokwisha ota kwenye jumla ya hekari 1800 na zingine 1300 za malisho katika kijiji cha mtanana Wilayani Kongwa kwa kufunikwa na maji, huku Afsa Mtendaji wa kijiji hicho akisema kuwa tayari kaya 5 zimesha hama kwenye makazi yao na wengine kushauriwa kufanya hivyo kutokana na hofu
Tags
MAFURIKO