BANDA MEDIA BLOG

RAIS MAGUFULI AJITOA SWALA LA KUONGEZA MUDA MADARAKANI



Dar es salaam: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa hana mpango wowote wa kuongeza kipindi cha muda wa kukaa madarakani kutoka miaka mitano(5) iliyo kwahivi sasa hadi saba (7) kama wanavyopendekeza wengine.

Akiongea kwa niaaba ya Rais Magufuli baada ya kumtembelea leo tarehe 13 Januari, 2018 ikulu Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole amesema kuwa Rais amemuelekeza kuwajulisha wanachama wa CCM na umma wa Watanzania kuwa anasikitishwa na hafurahishwi na mjadala unaoendelea juu kuongezwa kwa kipindi cha Urais kutoka miaka 5 iliyowekwa kwa mujibu wa katiba, hadi miaka 7"

Ndg. Polepole amesema Mhe. Dkt. Magufuli amewataka wanachama wa CCM na umma wa Watanzania kwa ujumla kuupuuza mjadala huo kwa kuwa haujawahi kujadiliwa katika kikao chochote cha chama, na ni kinyume na katiba ya CCM na katiba ya nchi.


Ameongeza kuwa Mhe. Dkt. Magufuli amewataka wana CCM na umma wa Watanzania kutokubali kuyumbishwa ama kupotoshwa na mambo yasiyokuwa ya msingi na badala yake wajielekeze katika ajenda muhimu ya kujenga uchumi na kutekeleza Ilani ya CCM ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Ndg. Polepole amebainisha kuwa Mhe. Dkt. Magufuli hana mpango wowote na hatarajii kuongeza kipindi cha Urais wakati wote wa uongozi wake.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG