SHIRIKA LA WAHAMIAJI IMESEMA NUSU YA WAKIMBIZI IRAQ WAMEREJEA KWAO
byJohn Banda-
0
Zaidi ya nusu ya wakimbizi wa Kiiraqi wamerejea makwao
Shirika
la Kimataifa kwa ajili ya Uhajiri (IOM) limetangaza kuwa hadi kufikia
mwishoni mwa mwezi Desemba wa mwaka uliomalizika wa 2017, wakimbizi
milioni tatu, laki mbili na 20 elfu wa Kiiraqi walikuwa wamesharejea
makwao.
Msemaji wa IOM Sandra Black ameashiria hatua
zilizochukuliwa na vikosi vya jeshi la Iraq za kuyakomboa maeneo
yaliyokuwa yamevamiwa na kukaliwa kwa mabavu na magaidi na kuboresha
hali ya usalama katika maeneo hayo na kueleza kwamba: hadi mwishoni mwa
mwaka 2015 ni wakimbizi laki tano tu wa Kiiraqi walikuwa wamerejea
kwenye makazi yao, lakini hadi kufikia mwishoni mwa mwaka uliopita 2017
idadi hiyo ilifikia milioni moja na laki nane na nusu.
Kwa mujibu
wa msemaji huyo wa Shirika la Kimataifa kwa ajili ya Uhajiri nchini
Iraq, theluthi moja ya wahajiri wa Kiiraqi waliorudi kwenye eneo la
makazi yao nyumba zao zote zilikuwa zimebomolewa kikamilifu. Sandra BlackHapo
kabla msemaji wa Wizara ya Uhajiri ya Iraq Sattar Nuruz alikuwa
ametangaza kuwa asilimia 45 ya watu walioathiriwa na vita wamerejea
kwenye makazi yao katika maeneo ya Mosul na Salahuddin huko kaskazini
mwa Iraq pamoja na Diyala na An Anbar, mashariki na magharibi mwa nchi.
Kwa mujibu wa Nuruz wakimbizi hao waliorejea makwao ni sehemu ya watu
milioni tano ambao tangu mwezi Juni mwaka 2014 walilazimika kuzihama
nyumba zao na kwenda kutafuta hifadhi kwenye makambi na maeneo ya
usalama