BANDA MEDIA BLOG

Singida United yatinga nusu fainali Mapinduzi Cup


Ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Mlandege umeifanya timu hiyo ya mkoani Singida kuwa ya kwanza kufuzu hatua ya nusu fainali ya Mapinduzi Cup baada ya kufikisha pointi tisa walizozipata kufuatia kushinda mechi tatu mfululizo katika Kundi B.

Singida United ilianza kombe la Mapinduzi kwa kuifunga Zimamoto 3-2, mchezo wa pili ikashinda 3-1 dhidi ya Taifa Jang’ombe kisha ikaifunga 3-0 Mlandege. Singida ambao ni wageni katika mashindano ya Mapinduzi wana wastani wa magoli sita (wamefunga magoli tisa na kuruhusu magoli matatu).
Mechi ijayo Singida inatarajia kushuka uwanjani kucheza dhidi ya JKU ukiwa ni mchezo wa nne kwa upande wa Singida.
Kundi B lina timu sita ambazo ni Singida United, Yanga (zote kutoka Tanzania bara), Mlandege,  Jang’ombe Boys na Zimamoto (zote za visiwani Zanzibar).

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG