
Mwalimu Muguru alihukumiwa kifungo hicho, Februari 21 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi Russy Mkisi, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka bila kuacha shaka.
Awali, Mwendesha mashitaka wa Polisi, Ramsoney Salehe, alidai mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa akiwa mtumishi wa umma, huku akitambua kufanya hivyo ni kosa, Februari 15 na 16, mwaka jana, kwa makusudi alimkamata Mhinda Kazimili (19) na kumfungia ndani ya nyumba aliyokuwa akiishi.
Aliitaja nyumba hiyo kuwa ni ya walimu iliyoko kwenye eneo la shule na kwamba baada ya kumfungia alimfanyia kitendo cha kumlawiti kwa siku mbili.
Mwendesha mashtaka alidai kuwa mtuhumiwa alipokwenda kazini, Mhinda alipata upenyo wa kutoroka na kukimbia nyumbani ambako alifika na kutoa taarifa kwa wazazi na Mtendaji wa Kata kisha mtuhumiwa akakamatwa akiwa kazini na kufikishwa mahakamani Februari 17, mwaka jana.
Kabla ya kutoa hukumu hiyo, Hakimu Mkisi alisema mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi watano wa upande wa mashtaka akiwamo daktari ambao haukuacha shaka yoyote na inamtia hatiani.
Hata hivyo, Hakimu huyo alimpa Muguru nafasi ya kujitetea ili kuishawishi mahakama impunguzie adhabu huku akiomba apunguziwe adhabu kwa kuwa anategemewa na wazazi wake pia amekuwa mahabusu kwa mwaka mmoja.
Mwendesha Mashitaka aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa kwa kuwa kitendo alichokifanya ni kujidhalilisha na akiwa mtumishi wa umma pia ameidhalilisha taaluma ya ualimu.
Hakimu Mkisi alimhukumu kwenda jela miaka 30 ili liwe fundisho kwenye jamii na wengine watambue vitendo vya kinyama havisitahili ndani ya jamii.
Tags
JELA