BANDA MEDIA BLOG

JAFFO AZINDUA KAMPENI YA KUPAMBANA NA RUSHWA NA MIMBA ZA UTOTONI KATIKA CLUB ZA WANAFUNZI WA MSINGI NA SEKONDARI AWTAKA WALIMU KUTUNGA NYIMBO ZA MCHAKA MCHAKA ZINAZOTAJA RUSHWA

Waziri TAMISEMI Suleman Jafo akifafanua jambo katika uzinduzi huo


Waziri Jaffo, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto  Wizara ya Afya Margeret Mussai wakiwa pamoja na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwenye uzinduzi huo, [PICHA NA JOHN BANDA WA BANDA BLOG]





Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM [UVCCM]Mkoa wa Dodoma Billy Chidambwa akisalimia katika uzinduzi huo

Mkurugenzi Mtendaji wa Creative Plan akizungumza kwenye uzinduzi huo

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto  Wizara ya Afya Margeret Mussai


NA JOHN BANDA, DODOMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Sulemani Jaffo amewataka walimu kote nchini kutunga nyimbo za Mchaka Mchaka watakazokuwa wakitumia wanafunzi zinataja Rushwa hali itakayowafanya watanzania kuchukia Rushwa kuanzia  wakiwa wadogo

Jaffo alitoa agizo hilo kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Kupambana na Rushwa na Mimba za Utotoni kupitia Club za wanafunzi wa Msingi na Sekondari mashuleni kampeni inayoendeshwa na Wizara ya Afya na Shiriki la Creative Plan [CP] 

"watoto hawa wakiwa wanaimba nyimbo za mchaka mchaka na huku wakiitaja rushwa na madhara yake kwa jamii ya Watanzania, itaeleweka zaidi na itasikika vizuri hata kwa wali ambao hawataki kiisikia masikiaoni mwao na hivyo itakuwa rahisi kuikabili watakapokuwa wakubwa walimu wasaidini", alisema 

 Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la CREATIVE PLAN Juma Mtewa alisema ni rahisi kumfundisha mtoto kuliko mtu mzima kwa kuwa Mtu mzima hawezi kuelewa kwa haraka kama ilivyo kwa mtoto

"Kazi hii ni muhimu sana kwa taifa tunamshukuru Waziri Jaffo kwa kuwatangazia Wakuu wa Mkoa ili watupe ushirikiano lakini imekuwa na changamoto kubwa kwa kuwa wengine wanajua kunakuwa na posho na tunapowambia ni kujitolea wanakimbia hapa tulipo tupo wenyewe viongozi mbalimbali walituacha lakini pia wapo wengine wanaojua kuwa tumekuja kuwachimba hivyo changamoto ni kubwa", alisema

Nae Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Afya Margaret Mussai aliwataka wazazi, walezi pamoja na jamii kwa ujumla kuhakikisha wanawaweka watoto kwenye uangalizi ili kuwaepusha na mimba za utotoni kutoka kwa watu wazima wanaoisha bila kufuata maadili ambao wamekuwa wakiwarubuni watoto kufanya nao ngono kwa vishawishi mbalimbali vikiwemo usafiri, chips na tupesa kidogo kwa ajili ya matumizi shuleni



Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG