BANDA MEDIA BLOG

KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA AWAFUNDA WACHUNGAJI NAMNA YA KUKEMEA DHAMBI MAKANISANI IKIWEMO KULINDA MAADILI KWA WAUMINI WAO

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gillis Moroto akifafanua jambo wakati alipokuwa akiongea na viongozi wa umoja wa madhehebu ya Kikristo Mkoani Humo

Mwenyekiti wa Umoja wa Madhehebu ya Kikristo Mkoani Dodoma Dkt, Damas Mukassa akizungumza jambo wakati alipokuwa akimshukuru kamanda polisi wa mkoa huo Gillis Moroto mara baada ya kumaliza mazungumzo na viongozi hao

Kikao Kamanda Moroto akiendelea kuzungumza na viongozi hao wa Madhehebu ya Dini ya Kikristo katika Bwalo la Polisi mjini Humo

Wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia kwa karibu mazungumzo hayo ambayo yalilenga ulinzi na maadili makanisani   [PICHA NA JOHN BANDA WA BANDA BLOG]










NA JOHN BANDA, DODOMA
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Moroto amewataka wachungaji kukemea vitendo vya uvunjifu wa maadili makanisani ikiwemo wanawake wanaovaa nguo fupi na za kubana huku akiwataka kulinda makanisa yao kwa kuweka Camera za CCTV

Moroto ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa madhehebu ya Dini ya Kikristo aliokutana nao katika Bwalo la polisi mjini humo .

Kamanda huyo alisema kuwa viongozi wa Makanisa wanatakiwa kukemea vitendo vya utovu wa maadili ili kuanzia kwa watoto mpaka kwa watu wazima wanaongia makanisani bila kujiheshimu hali itakayofanya taifa kuwa na watu wanaojitambua

"unakuta wanawake wanaingia makanisani wakiwa na nguo fupi, za kubana na zingine zimepasuliwa nyuma huku wengine wakiwa watoto wa wachungaji hayo ni maadili gani kemeeni vitendo hivyo
wengine wanashindwa hata kuwakea wake zao na watoto eti wanaendekeza ukisasa

Hata hivyo kamanda huyo amewataka viongozi wa makanisa kuweka ulinzi katika makanisa yao ili kuepukana na vitendo vya uhalifu vinavyoweza kujitokeza.

Kwa upande wao Viongozi wa Umoja wa Madhehebu hayo wameunga mkono agizo hilo huku wakiahidi kulifanyia kazi ambapo kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Madhehebu ya Kikristo Mkoa wa Dodoma Askofu Dkt, Damas Mukassa alisema wamepokea maelezkezo hayo ya Kamanda wa polisi na tayari yameshaanza kufanyiwa kazi...
Nae katibu wa Umoja huo Eliah Mauza alisema kwa upande wake yeye hakuitwa na Mungu kuwa mfanyabiashara bali kufanya kazi ya kuokoa Roho za watu ili waende mbingni na si kuwataka watoe sadaka hata kama wanavaa nguo fupi za kubana na milegezo kwa kisingizio cha utanashati au ukisasa.

"ni kweli sadaka ni nzuri na zifanya kanisa kuendelea lakini kupokea sadaka ya muovu haina maana  lazima kwanza mtu awe msafi moyoni mwake na usafi huo utaokeza na nje na ndipo akitoa sadaka inapokelewa, makanisa siyo mahali pa kushindania kutenda kinyume na maagizo ya Mungu", alisema




Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG