BANDA MEDIA BLOG

MKUU WA WILAYA YA BAHI AAGIZA KIJIJI KIPANDE MITI 25,400 AMBAPO KWA KATA NI MITI ELFU 70 AMBAYO ITIMZA IDADI YA MITI 1.5 MIL , LENGO LIKIWA KUUNGA MKONO AGIZO LA MAKAMU WA RAIS LA KUIJANISHA DODOMA



Mkuu wa Wilaya ya Bahi Elizabert Kitundu akipanda Mti wakati wa kampeni ya Upandaji miti katika wilaya hiyo kwa lengo la kuiunga mkono Serikali ambayo hivi karibuni ilitangaza kutaka kuubadilisha mkoa wa Dodoma kuwa wakijana kutokana na Miti.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Bahi Rachel Chuwa akipanda mti kati zoezi hilo
Mkuu wa Wilaya hiyo akisoma Hotuba kabla ya upandaji wa Miti Mbele ya watumishi wa Halmashauri pamoja na wananchi, kushoto Afsa Aridh wa Wilaya ya Bahi Chidieli Mrutu  [PICHA NA JOHN BANDA WA BANDA BLOG]

Afsa Tarafa wa Tarafa hiyo na hakuwa nyuma




NA JOHN BANDA, DODOMA
Katika kuunga mkono Agizo la Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan la upandaji wa miti ili kuukijanisha Mkoa wa Makao makuu ya Nchi – Dodoma  mkoa huo umeandaa mkakati wa kuzitaka Halmashari zote za Wilaya kupanda miti mil 1.5 ambapo ili kufanikisha zoezi hilo mkuu wa wilaya ya  Bahi Elizabert Kitundu ameagiza kila kata kupanda miti Elfu 70.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya zoezi hilo la upandaji wa miti uliyofanyika katika kijiji cha Bahi Sokoni ambapo viongozi mbalimbali walipanda miti Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa ili kufanikisha zoezi hilo inabidi kila kijiji kipande miti 25,400  kwa vijiji vyote 59
“mkoa umepanga siku hii ya feb 8 iwe siku maalum ya upandaji miti ktk kila wilaya ili kuunga mkono agizo la serikali na kwetu hapa tunatakiwa kupanda miti million 1.5 na naagiza kila kiongozi wa kata na vijiji atenge eneo la kupanda miti hiyo
Itakuwa kila nitakapotembelea naomba nionyeshwe miti iliyopandwa na kiongozi yoyote ambaye hata fanya hivyo hatutamvumilia”, alisema
Awali akizungumza katika uzinduzi wa mpango huo wa upandaji wa miti hiyo Afsa Aridh wa Wilaya ya Bahi Chedieli Mrutu amesema ili kuweza kutekeza kwa ufanisi agazo hilo tayari wameshaanza kushirikisha taasisi na mashirika mengine zikiwemo za Dini na Tasaf ambao tayari wameshaanza kupanda miti katika baadhi ya vijiji.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG