
WAZIRI wa
Nchi Ofisi ya waziri mkuu, Kazi, Ajira, vijana na walemavu Jenista Mhagama
amesema Serikali isingefanya maamuzi ya kuunganisha mifuko ya Hifadhi ya Jamii
sekta ya hiyo ilikuwa ina kwenda kufa.
Akizungumza
na wajumbe wa baraza kuu la Chama cha wafanyakazi wa Serikali za mitaa [Talgwu]
waliokutana mjini Dodoma kwa ajili ya mkutano wao wa mwaka Waziri Mhagama
amesema mfuko wa kwanza kufa ungekuwa PSPF ukifuatiwa na LAPF ambao ungekufa mwezi
Desemba mwaka huu kutokana na kukusanya 44 bil kwa mwezi wakati malipo ya
pensheni kwa mwezi ni 77 bil.
Aidha Waziri
huyo amesema moja ya faida atakazozipata mfanyakazi ni pamoja na kulipwa fedha
katika kipindi cha miezi 6 na pia kuweza kuzitoa fedha hizi na kuzihamisha
ambapo itakuwa ni faida mara mbili.
Awali
akiongea wakati akimkaribisha mgeni rasmi katika mkutano wa Baraza hilo
Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa Serikali za mitaaa [Talgwu] Suleiman
Kikingo ameainisha shuhuli za mkutano huo wa mwaka uliowakutanisha wajumbe toka
mkoa yote ya Tanzania Bara
Tags
TALGWU











