BANDA MEDIA BLOG

WANAFUNZI WA KITIVO CHA ELIMU CHUO KIKUU CHA DODOMA SASA KUJITOLEA KUFUNDISHA KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ILI KUINUA ELIMU MKOANI HUMO TOKA NAFASI YA PILI TOKA MWISHO MPAKA NAFASI YA KWANZA

Jengo la Utawara Chuo kikuu cha Dodoma

Mwanzilishi na Mratibu wa kujitolea kufundisha mashuleni toka Collage ya Elimu ya Chuo kikuu cha Dae es salaam [UDZM]  Emijidius Cornel akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika viunga vya chuo kikuu cha Dodoma [UDOM]
Rais wa Shirikisho la wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma Fransisco Zalalila akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo kuhusu mpango wa kuanzisha tawi la kujitolea kufundisha masomo ya sayansi na hesabu mashuleni [PICHA NA JOHN BANDA WA BANDA BLOG]



NA JOHN BANDA, UDOM
Wanafunzi wanaosomea Ualimu katika chuo kikuu cha Dodoma [UDOM]  wametakiwa kuacha kuchati kwenye Mitandao ya Kijamii kwa ajili ya mambo yasiyofaa yakiwemo mapenzi badala yake waende kwenye shule zilizopo pembezoni mwa chuo hicho kujitolea kufundisha wanafunzi.

Hayo yamesemwa na Mwanzilishi na Mratibu wa wanafunzi wa kujitolea wa kitivo cha Elimu Chuo Kikuu cha Dar es- salaam Emijidius Cornel wakati akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa Chuo kikuu cha Dodoma kwa lengo la kuanzisha tawi la mpango huo wa kujitolea katika ufundishaji wakati wanapokuwa hawana vipindi.

Cornel alisema kuwa katika Collage hiyo  iliyopo UDZM walianza wakiwa wanafunzi 10 na kufikia 400 kwa sasa ambapo wanajitolea kufundisha masomo ya Sayansi na Hesabu katika shule za Ilala jijini Dar es salaam  na hivyo ujio wake Dodoma ni ili kuanzisha ushirikiano na UDOM
"unajua unaweza kufikili kuna ugumu kujitolea kwenda kufundisha kwa sababu sisi ni wanafunzi wa elimu ya juu hapana hakuna ugumu wowote kwa sababu tunatumia nafasi zile ambazo hatuna vipindi au kama tuna kupindi kimoja tukimaliza tunaenda kujitolea kufundisha wadogo zetu

"kuna faida kwa mwanafunzi wanaosoma Elimu ya juu kujitolea kufundisha watoto wa shule zinazozunguka Chuo kwa kuwa wanapata uzoefu wa kile wanachosomea kuliko kusubili masomo ya vitendo pekee pia tunashauri wanafunzi wanaosomea fani zingine kwenda kujitolea kutokana na fani zao ili wapate uzoefu", alisema
  
Kwa upande wake Rais wa wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma Fransisco Zalalila alimesema anasikitishwa na Mkoa huo kuwa duni kielimu nchini wakati kuna vyuo vingi vya Elimu ya juu hali inayosababishwa na kutokana kwa taasisi hizo za kielimu kwenda kusaidia jamii inayowazunguka

"ona mkoa wa Dodoma ambao una vyuo vingi vya elimu ya juu lakini bado ufaulu wa wanafunzi wa msingi na sekondari upo chini kitaifa hali hii haikubaliki imefika wakati wanafunzi wa vyuo kujitoa tukawafundishe kwa kujitolea ili kuinua ufaulu ", aliema

Aidha alisema mara baada ya kumaliza mazungumzo na uongozi wa chuo ambao watakutana kuwapa pendekezo lao itawabidi kuuona uongozi wa mkoa kupitia mkuu wa mkoa ili waweze kupata sapoti itakayowarahisishia kufanya kazi hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG