
Kubenea ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kinondoni na kubainisha kuwa kwa sasa umezuka mtindo kwa watumishi wa umma kugombana na wabunge wa upinzani ili wapandishwe vyeo.
Ameongeza kuwa ni kweli amefukuzwa katika ofisi hizo na kwamba tayari amekwishapata ofisi nyingine katika eneo la ubungo maeneo ya majengo ya urafiki.
Hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Happi aliwafukuza katika ofisi zao wabunge wote walikuwa wakitumia jengo la mkuu wa wilaya kwa madai kuwa anataka kuzitumia ofisi hizo kwa matumizi ya serikali.
Tags
KUBENEA