Akiongea leo March 6 kupitia ukurasa wake wa twitter Lema alianza kwa kuhoja kauli hiyo hivi ni kweli tunahitaji Kamati teule kuhusu utekaji na kufifia kwa demokrasia Nchini ?
Lema anaona si kusudio mahususi na la Busara kwa kuwa yanayotokea kwa sasa nchini ni maamuzi ya chama Tawala ccm katika mikutano yake ya ndani ya Bunge na nje ya Bunge kuhusu hali ya demokrasia na siasa Nchini, ujenzi wa vyama vya siasa na mikutano imepigwa marufuku, Mikutano ya Bunge live pia imepigwa marufuku , Wabunge na Madiwani wa Upinzani waneendelea kupitia mateso makubwa,vitisho vya mauaji , kuwekwa mahabusu na kufungwa.
Lema anasema kuwa Wakati mambo haya yanaendelea kutokea Bunge la Tanzania limekataa hata kulipia matibabu ya Mh Lissu.
Hakuna Mbunge mmoja wa ccm akiwemo Husein Bashe alishawahi kwenda kumjulia hali Mh Lissu Hospital, unajiuliza ni kwa nini ?" alihoji Lema
Lema amesema kuwa Mambo haya yako wazi na kwamba hayahitaji PHD kujua msimamo wa Wabunge wa ccm kuhusu haki,ukweli na nuru ya mabadiliko .
"Wabunge wa ccm wakibadili mtazamo kuhusu Nchi Bunge litakuwa imara na Bunge imara ndio msingi wa Serikali bora na Bunge imara linatokana na Wabunge majasiri, wako wapi ndani ya ccm ?
Msingi wa kwanza wa ukomavu wenu ni kurudisha hadhi ya Bunge kwa umoja na idadi yenu , platform nyingine nje ya kujitathimini kwa masilahi ya Nchi ni unafiki.
Bashe unafikiri Kamati teule inaweza kuwa na maana kwenye Bunge hili ? hotuba za Wapinzani Bungeni zime endelea kuwa sensored ndani ya Bunge na haya ni maoni mbadala ya ushauri kwa Serikali lakini siku zote mmekaa kimya." aliandika Lema kwenye ujumbe wake
Mbunge huyo wa Arusha mjini aliendelea kumwambia Bashe kuwa Chama chake ndio tatizo na Viongozi wake, na yeye kama Mbunge anafahamu mambo haya, "hivi kweli tunahitaji tena kugundua kanuni ya kutengeneza gari wakati kuna magari yana tembea barabarani ? "
Tunahitaji umoja wenu kwa masilahi ya haki ndani ya Bunge kwenye mambo yote yanayo rudisha heshima ya Wabunge , wingi wenu umekuwa hasara kwa Nchi badala ya faraja.
"Tunapoona maigizo yanayotaka kupotosha haki yanazingatiwa hapa ndipo tunapatwa hasira na kuondoa nidhamu katika mahusiano yasiyo na tija na Nchi , hata hivyo andiko hili sio ugomvi lakini pia limejengwa hasira na hali zetu kisiasa tunayopitia, sisi Wabunge wa upinzani karibu wote tuna kesi sehemu mbali mbali Nchini, mmoja wetu sasa ni mfungwa (Sugu) .
Tunapitia maumivu makali sana kwa sasa hatuitaji tena sinema." alisema Lema Kwa upande wake Mbunge wa Kigoma mjini Zitto kabwe ameonesha kuunga mkono wazo la Bashe na kusema kuwa linapaswa kuungwa mkono "Uamuzi huu wa Mbunge wa Nzega Mjini ni uamuzi sahihi unaopaswa kuungwa mkono na kila mmoja wetu. Kwame Nkrumah alipata kusema “ One Struggle, Many Fronts “. Kila mtu anayefanya lolote kusaidia kuiokoa nchi yetu aungwe mkono bila kujali Chama chake. Nitaunga mkono hoja hii ikija"
Naye waziri wa Maliasili na utalii Hamisi kigwangalla ameonesha kuunga mkono wazo hilo "Viongozi vijana ama wa ‘cohort’ yetu tuko bize kuangushana badala ya kuungana mkono kwenye jitihada za kutafuta suluhu za changamoto zinazoikabili nchi yetu; kuna changamoto za ajira, usalama wa chakula, mabadiliko ya tabia nchi na kadhalika. Tupambane na hizo siyo na Kigwangalla" alisema kigwangalla
Tags
Bashe