BANDA MEDIA BLOG

MBUNGE MWANAMKE AWASHUKIA WANAWAKE



Mbunge wa viti maalum mkoa wa Dodoma Fatma Tawfiq amewashukiwa wanawake kwa kusema jukumu la kuwatetea wanawake linabaki kwao wenyewe ,hususani kuwasaidia wanawake walioko maeneo ya vijijini ili waweze kujitokeza katika shughuli mbalimbali na kufanya maamuzi kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa .

Fatma ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika kata ya msalato iliyopo nje kidogo ya manispaa ya Dodoma.
Ameongeza kuwa wanawake wanapaswa kujiwezesha katika maeneo ya kiuchumi kisiasa na kijamii ili wapate fursa ya kushiriki katika maamuzi mbalimbali hatimaye yaweze kuwaletea tijana mafanikio.

Awali akisoma Risala kwa Mgeni rasmi Katibu wa Jukwaa la muwezeshaji wanawake kiuchumi mkoa Elizabert Mtimi amesema kuwa changamoto kubwa wanayokabiliana nayo nikwa taasisi za kifedha ambazo zimekuwa zikitoza riba kubwa ambazo zimekuwa ni kikwazo kwao katika marejesho ya mkopo huo nakuwa kero na karaha na kuongeza ukali wa maisha kwa mkopaji.
Kwa upande wake msimamizi mkuu wa kitengo cha damu salama ya mkoa Dr Leah Kitundya amewahamaisha akina mama kutokuwa nyuma katika zoezi lakuchangia damu ili kuwasaidia akina mama wenye uhitaji wa damu .
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni kuelekea uchumi wa viwanda,tuimarishe usawa wa jinsia na uwezeshaji wa wanawake vijijini.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG