BANDA MEDIA BLOG

MIGOGORO YA NDOA HUTOKANA NA WANAWAKE WAJASIRIAMALI.



 Wanawake wametakiwa kuwa waaminifu kwa waume zao ili kuepusha migogoro ya ndoa na kuleta heshima katika familia .

Hayo yameelezwa leo mjini hapa na meneja wa mradi wa shirika la viwanda vidogovidogo (SIDO) Bonifance Ndungulu alipokuwa akizungumza na kituo hiki.

Ndungulu amesema migogoro mingi inatokea kwa baadhi ya wanandoa kutokana na wanawake wajasiriamali kufanyabiashara kwa kutembeatembea katika nchi mbalimbali nahii inapelekea wanawake kutokuwa waaminifu kwa waume zao.
Akifafanua zaidi Ndungulu amesema kuwa Katika mizunguko kama hiyo,inawasababisha akina Mama wenye tama,na wale wasiokuwa waaminifu, wamekuwa wakitumia fursa hiyo, kuwapata mabwana wengine, lengo kubwa ikiwa kujipatia fedha mbadala na starehe.
Akizungumzia suala la ndoa mchungaji wa kanisa la kilutheri (KKKT), lilipo Ihumwa mjini hapaamesema kuwa hivi sasa ndoa nyingi uvujika,kutokana na uwaminifu kupotea,hasa kwa baadhi ya Wanawake wanaopata mapato mabuwa kuliko Waume zao.
Aidha ameongeza kwa kusema tabia hizo kwa akina mama hao, kunawafanya wanaume zao kuona nyumba zao kama gereza na matokeo yake hujiingiza mambo hatarishi ikiwemo kuingia katika ulevi, kuwa na nyumba ndogo ambapo hupelekea kusahau familia zao.
Lengo la Sido ni kuwawekeawajasiriamalimazingira mazuri ya kibiashara , kuwapa mafunzo ya kibiashara, kuwatafutia masoko na kuwaunganishana wajasirimali Mikoani na hata walioko nchi za jirani.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG