Amesema hayo leo Machi 5, 2018, Kupitia ukurasa wake wa twitter Nape ameandika kuwa ni lazima ushetani huo upingwe kwa nguvu zote hasa na vijana kabla haujaota mizizi na kusambaa. “Huu ulevi wa baadhi ya viongozi wa Afrika kutamani na kubadili ukomo wa wao kuwa madarakani ni ushetani na lazima upingwe kwa nguvu zote hasa na vijana kabla utaratibu huu haujaota mizizi na kusambaa! Hii ni zaidi ya kansa!” aliandika Nape
Nape amewahi kuwa waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kabla ya kuvuliwa wadhifa huo na Rais John Magufuli na nafasi yake kuchukuliwa na Dk Harrison Mwakyembe tulipompigia Muakilishi.com amekiri kuwa twitter ni yake ingawa hakuwa tayari kufafanua zaidi.
Tags
Nape Nnauye