Simba walianza kupata goli dakika ya 10 baada ya mchezo kuanza kwa mkwaju wa penati uliofungwa na John Bocco baada ya mlinzi wa Al Masry Mohamed Koffi kushika mpira kwenye box wakati akiwa kwenye harakati za kuokoa. Goli hilo halikudumu dakika moja baadaye al masry wakasawazisha kupitia kwa Mohamed Ahmed.
Dakika ya 26 Al Masry walipata mkwaju wa penati kufuatia mlinzi wa simba James Kotei kuunawa mpira kwenye box, mkwaju huo wa penati ukakwamishwa kambani na Ahmed Abdalrauf lakini simba wakasawazisha kwa mara nyingine wakipata tuta baada ya Mohamed Koffi kuushika mpira wakati akijaribu kumzuia Okwi.
Tags
SIMBA SC