BANDA MEDIA BLOG

WAZIRI AKERWA NA WAFUGAJI KUUWA FISI,SIMBA NA NDEGE KWA KUWEKEA SUMU KATIKA NYAMA.



 Waziri wa maliasili na utalii Dk Hamisi Kigwangalla akizungumza jambo  wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanyamapori Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere mjini Dodoma

Mwenyekiti wa Rafiki Wildlife Foundation,Mchungaji Clement Matwiga, akiongea jambo  na wakazi wa Dodoma waliohudhuri Maadhimisho hayo wakati alipokuwa akisoma Risala
Kaimu Meneja Uhusiano wa Mamraka ya Hifadhi ya Ngorongoro Joyce Mgaya akizungumza jambo wakati Waziri wa maliasili na utalii Dk Hamisi Kigwangalla alipotembelea Banda lao la maonyesho katika viwanja hivyo

Mhifadhi Misitu wa Maliasili Dodoma [TFS CENTRAL ZONE]  Charles Tuyi  akimkabidhi Waziri huyo zawadi ya asili inayozalisha katika ukanda huo wakati aliotembelea banda lao la maonyesho
Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Wanyamapoli  wala Nyama Dkt, Dennis Ikanda akieleza Changamoto zinazowakabili wanya hao [PICHA NA JOHN BANDA WA BANDA BLOG]








Waziri Kigwangala akipanda mti kwenye viwanja vya Nyerere mara baada ya kumaliza kuhutubia katika maadhimisho hayo

Picha ya pamoja na wanafunzi waliohudhulia katika maadhimisho hayo
NA JOHN BANDA, DODOMA
 Waziri wa maliasili na utalii Dk Hamisi Kigwangalla amekerwa na kitendo kilichofanywa na wafugaji wa pembezoni mwa hifadhi ya Ruaha kwa kuwaua Simba 6,Fisi zaidi ya 100 na Ndege 100 kwa kuwatilia sumu katika nyama.

Akizungumza  mjini Dodoma wakati Maadhimisho ya Siku ya Wanyamapori Duniani Dk Kigwangalla alisema kitendo kilichofanywa na wafugaji cha kuwaua paka wakubwa kwa kulipiza kisasi takribani wiki tatu zilizopita kimeikera Serikali.
“Kitendo cha jamii ya wafugaji pembezoni mwa hifadhi ya Taifa ya Ruaha kuweka sumu katika nyama na kuwaua takribani Simba 6,Fisi zaidi ya 100 na ndege waliokuwa mzoga zaidi ya 100,’’ameeleza.
Akifafanua zaidi amesema Vitendo kama hivi vimekuwa vikijitokeza katika maeneo mbalimbali ya Nchi yetu hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika na kudai kuwa hata kama watachukuliwa  hatua lakini tutakuwa tumepoteza idadi kubwa ya wanyama ambao tulipaswa kuwahifadhi.
Mbali na hayoWaziri Dk Kigwangalla ametoa wito kwa jamii hususan wafugaji kuwakinga na kuyalinda makundi ya jamii ya Paka wakubwa pamoja na kutunza mazingira.
Waziri Kigwangalla amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuamsha uelewa kwa jamii juu ya uhifadhi na umuhimu wa wanyamapori na mazingira.
“Katika siku za karibuni tumeshuhudia kutoweka kwa baadhi ya wanyamapori kama faru na Tembo aidha wanyamapori jamii ya Paka wakubwa,ambao ni Simba,Chui na Duma pia wanafuatia katika hatari ya kutoweka,”amesema
Hata hivyo Dk Kigwangalla amesema kwa mujibu wa Taasisi ya Wanyapori (Tawiri) Tanzania kuna Simba 16800,Chui 25,000 na Duma 1180.
Alisema wanyapori wa Jamii ya Paka wakubwa ni kivutio kikubwa cha utalii na hivyo kuliingiza taifa fedha nyingi.
“Takwimu zinaonesha kwamba biashara ya Utalii inachangia asilimia 18 ya pato la Taifa asilimia 25 ya fedha za kigeni,ajira 500,000 za moja kwa moja na ajira zaidi ya milioni mbili ambazo sio za moja kwa moja zimepatikana,”amesema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Rafiki Wildlife Foundation,Mchungaji Clement Matwiga,amesema wataendelea kutoa elimu juu ya uhifadhi wa wanyamapori na mazingira.
“Kwa kushirikikiana na Mamlaka ya usimamizi ya Wanyamapori Tanzania(Tawa) elimu ya uhifadhi imetolewa kwenye kijiji kinachopakana na mapori ya akiba ya Mkungunero na Swagaswaga,”amesema.
Awali akizungumza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga amesema Serikali itaendelea kushughulikia migogoro inayojitokeza ya wananchi kuvamia hifadhi za Taifa.
 Akisoma Risala Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Wanyamapoli  wala Nyama [Tawiri] Dkt, Dennis Ikanda alieleza kuwa wanyama hao wapo katika hatari ya kutoweka katika sura ya Dunia ikiwemo Tanzania zikiwemo changamoto za kiuhifadhi, mabadiliko ya Ardhi katika maeneo wanayoishi, upatikanaji wa Chakula, uhalibifu wa mazingira hali inayosababisha kupungua kwa uwezo wa kuzaliana na tishio la Binadamu ikiwemo migogoro ya wafugaji na wakulima

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG