MBUNGE wa Ubungo – Dar es Salaam, Saed Kubenea akichangia hoja bungeni
leo kuhusu Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano inayosimamiwa na Profesa
Makame Mbarawa, ameomba ufafanuzi kutoka kwa Waziri Mbarawa akidai juu
ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limefunguliwa kesi nchini Uingereza
kutokana na deni la Tsh. Bilioni 80 hali ambayo amedai inaweza
kusababisha ndege za Bombadier kukamatwa.
Hayo amesema leo Bungeni, Aprili 24, 2018, na kuongeza kuwa tayari
Serikali ya Tanzania imelipa malipo ya awali kwa mawakili kwa ajili ya
kesi hiyo.