"Serikali baada ya kuona kumekuwa na changamoto kubwa sana katika utambuzi wa makundi maalum ambayo wengi wamekuwa wakiathirika na ugonjwa wa TB na UKIMWI. Hivyo tumeamua kujielekeza kutoa elimu kwa njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari lakini vilevile tuna mkakati mahususi wa kuwatafuta wagonjwa wa TB katika migodi sambamba na hilo tumetengeneza tumetengeneza mikakati jumuishi kati ya ugonjwa wa TB na UKIMWI", amesema Dkt. Ndugulile.
Pamoja na hayo, Dkt. Ndugulile ameendelea kwa kusema "sasa hivi tumeanza kujielekeza mahali kwenye watu wengi ili tuweze kuwapata kwa pamoja hususani wanaume ambapo mara nyingi wanakuwa katika bar. Msishangae kutuona na sisi tunapita huko kuwaomba kufanya upimaji wa suala la ugonjwa wa UKIMWI pamoja na TB".
Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile amesema kumgundua mgonjwa wa TB mapema na kumuweka katika matibabu ndio njia kuu ya kupambana na kulishinda tatizo la kifua kikuu jambo ambalo lipo kwenye mikakati ya serikali katika kufufua uwezo wa kufikia watu wote wanaohitaji huduma za TB ili kuwagundua mapema na kuwatibu kikamilifu.
Tags
Ukimwi naTB
