| Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ kulia akimnoa bondia Vicent Mbilinyi kwa kumuelekeza kupiga ngumi ya mkunjo wa chini ‘Upcat’ Mbilinyi anajiandaa na mpambano kati yake na Hussein Shemdoe utakaofanyika katika ukumbi wa Musoma Bar siku ya Mei Mosi Picha na SUPER D BOXING NEWS |
BONDIA Vicent Mbilinyi amendelea na mazoezi ya kumkabili
Hussein Shemdoe wakati wa mpambano wao utakaofanyika mei mosi siku ya
sikukuu ya wafanyaklazi Duniani mpambano huo utafanyika katika ukumbi wa
Musoma Bar uliopo Tandika Mwembe Yanga ambao utakuwa ni wa raundi 8
Mbilinyi anaenolewa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa
masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ amekuwa nje ya ulingo kwa muda
wa mwaka mzima sasa tangu mwishoni mwa mwaka 2016 na sasa anakuja
kivingine katika masumbwi.
Mbali na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano
mengine ya mabondia mbali mbali ambapo bondia Shafii Ramadhani
atapambana na Antony Mathias wakati Nassibu Ramadhani atavaana na Hamisi
Mohamed na Shomari Galibu atapambana na Hashimu Sheni wakati Said
Mluguru atavaana na Said Bakari ‘Kidedea’
Mapambano haya yote yatafanyika siku hiyo katika ulingo
mpya wa mdau wa masumbwi nchini Zahoro Maganga ‘Super Diego’ aliejenga
ulingo huo kwa ajili ya kuwakomboa mabondia kutokana na adha ambayo
imekuwa ikijitokeza kwa upande wa vifaa vya mchezo huo nchini.
Tags
BOXING