BANDA MEDIA BLOG

MGOGORO WA ARDHI BUIGIRI-CHAMWINO DODOMA....... DIWANI AMTEGA MKURUGENZI


 

PICHA NA HABARI NA JOHN BANDA, DODOMA
Diwani wa Kata ya Buigiri, Wilaya ya Chamwino, Mkoani Dodoma Mhe. Kenneth Yindi ametoa wiki mbili kwa Kamati ya Maboresho ya Makazi ya Kijiji cha Buigiri iweze kumpelekea taarifa juu ya matumizi ya fedha zaidi ya milioni 12 zilizochangwa na Wananchi zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Akizungumza katika Mkutano Maalumu wa kusikiliza kero za Wananchi juu ya mgogoro wa ardhi kati ya Kijiji cha Buigiri na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino uliodumu kwa miaka tisa Mhe. Yindi amesema anahitaji kupata ufafanuzi juu ya fedha hizo zilivytumika mpaka sasa ikiwa ni pamoja na kupata stakabadhi za malipo mbalimbali yaliyofanywa kwa ajili mradi wa Maboresho ya makaazi vinginevyo fedha hizo zirejeshwe na sheria ichukue mkondo wake

“haiwezekani wananchi wa wajibane kwa kuacha kufanya mambo yao mengine ya kimaisha wanachanga pesa kwa kujinyima wakidhani zinawasaidi kwa wakati lakini cha ajabu tangu wamechanga zaidi ya mwaka mmoja uliyopita mpaka sasa hakuna matokeo yoyote yaliyo wazi na yenye tija kwa ajili ya makaazi  yao
 

Sasa natoa wiki mbili mchanganuo wa matumizi pamoja na stakabadhi za fedha za wananchi zaidi ya 12 mil  tuwe tumeupata toka halmashari  vinginevyo tuone hatua  nyingine za kuchukua”, alisema
AIDHA Diwani huyo amesema kuwa imefika wakati wanachi wa Buigiri waruhusiwe kufanya kazi na Makampuni yanayojihusisha na upimaji Ardhi  ambayo yanaweza kutumia muda mfupi kuwapimia wananchi kama ilivyo kwa halmashauri nyingine ikiwemo halmashauri ya jiji Dodoma ambalo kwa kiasi kikubwa imefanikiwa katika upimaji ikiwemo kuondoa migogoro na wananchi kuhusu Ardhi 








Kutokana na swala hilo kumgusa Afisa Ardhi na Maliasili Halamshauri Wilaya ya Chamwino Rugambwa Banyikila ambaye Ofisi imekuwa ikifanya kazi na Kamati ya Maboresho ya Makaazi amesema fedha hizo hazijapotea wala kutumika vibaya hivyo yuko tayari kuonesha mchanagnuo wa matumizi yake pamoja na stakabadhi zote kwani zipo kwenye faili la kumbukumbu za mradi husika.
Hata hivyo mgogoro huo ambao umedumu kwa takribani miaka tisa umeonesha tumaini la kupata ufumbuzi baada ya Ofisi ya Mkurugenzi Wilaya ya Chamwino kukubali mapendekezo kutoka kwa Wananchi wa Kijiji cha Buigiri kutafuta Makampuni yatakayofanya kazi ya kupima Ardhi kwa kushirikiana na Kamati Maalumu ya Wananchi, zoezi ambalo kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Athuman Masasi halitachukua zaidi ya Mwezi mmoja kutoka leo  mei 16,2018.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG