Ruge Mutahaba ambaye ni Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media
Group ni miongoni mwa washiriki waliosimama kutoa darasa katika semina
ya Wanafunzi wa chuo kikuu Dodoma (UDOM) iliyofanyika katika ukumbi wa
Chimwaga lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kubadilisha fikra na
kutimiza wajubu wao katika sekta ya elimu na jamii kwa ujumla.
“Tukae tuambiane ukweli, matatizo ya kwetu sisi ni kitu cha kujivunia
kwasababu ndio sehemu ya kujipatia. Kwanini hakuna mtu humu ndani
anaanzisha kitu ambacho kinabeba na kinaweka wasanii wote na kutengeneza
pesa? Tuache kulalamalalama”- Ruge Mutahaba