TAASI YA UTAFITI WA KILIMO TANZANIA (TARI) YAJIDHATITI KUOKOA MABILION YANAYOPOTEA KILA MWAKA KUAGIZA MAFUTA YA KULA NJE
Mtafiti wa kilimo toka Idara ya usambazaji wa Teknolojia na uhusiano Hamis Amanje akionyesha mkungu wa mchikichi uliozalishwa na mbegu bora aina ya TENERANa John Banda, Dodoma
KATIKA kuhakikisha kuwa kiasi cha fedha Zaidi ya
bil. 3 zinazotumiwa na serikali kuagiza mafuta nje zinaokolewa Taasisi ya
utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) imebuni na kutengeneza mbegu ya mchikichi
aina ya TENERA ambayo kwa sasa inazalisha mafuta kwa wingi tofaiti na awali
Kauli hiyo imetolewa na Mtafiti wa kilimo toka Idara ya
usambazaji wa Teknolojia na uhusiano Hamis Amanje wakatai akiongea na waandishi
wa habari katika uwanja wa jamhuri jijini Dodoma ambako taasisihiyo inashiriki
maonyesho ya Ubunifu MAKISATU ambapo amesema hivi sasa uzalishaji wa mafuta
aina ya mawese umeongezeka.
Amanje amesema mbegu ya TENERA ni bora kwa sababu
miche yake inaanza kuzaa na kukomaa kati ya miaka 3 hadi mine toufauti na mbegu
ya awali ambayo ilikuwa ikitumia miaka 5 hadi 6 huku mbegu zake zikitoa mafuta
kidogo.
Amesema tangu mbegu hiyo ilipobuniwa na kuanza
kutumika mwaka 2018 uzalishaji wake umeongezeka kwa kipindi cha miaka mitatu
mpaka kufikia tani 4 mpaka 6 kwa hekta moja na kwamba mafuta ya kula nchini
yanapatikana kwa Zaidi asilimia 60 na mapambano yanaendelea ili kufikia
asilimia Zaidi ya 100.
mafuta bora ya mawese
Ameongeza kuwa usambazaji wa miche bora ya
michikichiki unaendelea kwa kushirikiana na wadau kuzifikisha katika
halmashauri za wilaya katika mikoa mbalimbali ambapo kwa sasa baadhi ya mikoa
ikiwemo ya Tabora, Mbeya na Kigoma zimeshafika
“kwa sasa mapambano yanaendelea ili tuweze kutimiza
malengo ya serikali ya kuzalisha mafuta ya kula hapahapa nchini kwa Zaidi ya
asilimia 100 toka asilimia 60 mpaka 70 za sasa ambapo fedha hizo bil 3.6 ambazo zimekuwa zikitumika
kuagiza mafuta nje zifanye kazi nyingine za maendeleo ya wananchi”, amesema
Aidha amewataka watanzania wanaozalisha miche
kutumia njia rahisi ya mapipa ambayo yanatunza joto kwa kuweka mavumbi ya mkaa,
majani na aina nyingine ya takataka ili kuepuka hasara ya kununua mashine za
uoteshaji ambazo zinapataika kwa garama kubwa
huu ni mkungu wa Mchikichi wa mbegu ya zamani ambayo huzaa mkungu mdogo unaotoa mafuta kidogo.
MAONYESHO YA WIKI YA KITAIFA YA SAYANSI, TEKNOLOJIA
NA UBUNIFU (MAKISATU), 2022 INAONGOZWA NA KAULI MBIU ISEMAYO “UBUNIFU KWA
MAENDELEO ENDELEVU”,