BANDA MEDIA BLOG

No title

 

WAMILIKI WA ARDHI WATAKIWA KULIPA KODI YA PANGO




Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inawajulisha wananchi kuwa kwa  Mujibu wa Sheria ya Ardhi (SURA ya 113) kifungu cha 44  kila mmiliki wa Ardhi anatakiwa  kutimiza  masharti ya umiliki ikiwa ni pamoja na sharti la kulipa kodi ya pango la ardhi kila mwaka.

Aidha, baadhi ya wamiliki wamevunja sharti hilo Kwa mujibu wa kifungu cha 45 la kulipa kodi ya pango la ardhi kwa wakati.

Hivyo, ninatoa taarifa kwamba, wananchi wote wanaodaiwa kodi ya pango la ardhi wanapewa nafasi ya mwisho kulipa kodi ya pango ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya tangazo hili. Baada ya muda huo kupita taratibu za kisheria za ubatilisho wa miliki zitaendelea.

IMETOLEWA NA DR. ALLAN KIJAZI KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI  

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG