MKUU WA WILAYA YA DODOMA MJINI AWATAKA WANAMAZOEZI KUMWAGILIA MOYO KWA STEP ILI KUEPUKA VIFO NA MAAMBUKIZI YA UKIMWI
wanamakao makuu wakishiriki mbio hizo za mazoezi
mkuu wa wilya ya Dodoma mjini Jabiri Shekimweri mwenye kapelo nyekundu akikimbia pamoja na wanajogging wa Ilazo, Dodoma Runners, Makao makuu Fitness Club na FFU kwenye mbio za km 10
Kamishna wa jeshi la Polisi, Charles Mkumbo akizungumza jambo mara baada ya kumaliza mazoezi hayo
Mkuu wa Wilaya akiwapa zawadi ya pongezi watoto hawa walio chini ya mikao 10 kwa kumaliza km zote 10
Makamu Mwenyekiti wa Makao Makuu Fitness Club Ernest Moses akipokea zawadi ya ushiriki wa mbio hizo zilizoandaliwa na DODOMA RUNNERS, toka kwa Dc
........................................................................................
NA JOHN BANDA, DODOMA
MKUU wa Wilaya ya Dodoma mjini, Jabiri Shekimweri amesema Kuelekea mwisho wa mwaka watanzania watunze
Afya zao kwa kuendelea kufanya mazoezi
Shekimweri ameyasema hayo wakati aliposhiriki na kumaliza mbio
za km. 10 zilizoandaliwa na DODOMA RUNNERS
Dc amesema “ni vizuri wanamazoezi kujichunga hasa kipindi hiki
tunapoelekea mwishoni mwa mwaka kwa kufanya mazoezi na kuepuka kumwagilia moyo
kwa kupindukia, tusipitilize tukaja poteza maisha au tukapata ukimwi”, amesema
Kwa upande wake Kamishna wa jeshi la Polisi, Charles Mkumbo amesema
mwishoni mwa mwaka huwa kuna mambo mengi yakiwemo ya kusafiri kutoka mkoa mmoja
kwenda mwingine hivyo kila mtu ajichunge
Kamishna Mkumbo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Timu ya Polisi
Tanzania inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC
Amesema “mwisho wa mwaka kuna mambo mengi hivyo unaposafiri hakikisha
unakwenda kwa mwendo wakawaida na watahadhali unapokuwa njiani kisha kasalimie
wazazi na wakati wa kurudi rudi salama ili tuukaribisha mwaka vizuri”, amesema
Aidha katika tukio hilo Jamila Awadh ameibuka mshindi na
kupewa zawadi baada kukimbia km. Zaidi 1,678 kwa mwaka huu wakati kwa upande wa wanaume aliyeibuka
mshindi wa kwanza kwa kukimbia KM.4,640
kwa mwaka huu wa 2022 ambaye ni sawa na kwenda Mkoani Dar es laaam mara 10 kwa
mguu
Vilabu waalikwa vya Jogging ambavyo vimeshiriki Mbio hizo ni
pamoja na Makao Mkuu Fitness Club, Ilazo Jogging, Kikosi cha Kutuliza Ghasia
cha Ffu Dodoma na Waandaaji Dodoma Runners