MWANGA AWATAKA VIONGOZI WA CCM KATA NA MATAWI KUFANYA VIKAO VYA KIKANUNI, WENYEVITI WA MITAA NAO WATAKIWA KIJITATHINI
BANDA MEDIA ONE, DODOMA
JUMUIYA ya Wazazi ambayo ni Jumuiya mama ya Chama cha
Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Dodoma mjini imefanya ziara ya kutembelea Kata
Mbalimbali za wilaya hiyo na kutoa maagizo kadhaa Kwa viongozi wa chama hicho..
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Stiven Mwanga akiongea hivi
karibuni mara baada ya kumaliza kutembelea Ujenzi wa vyumba vya madarasa na
maabara katika shule ya sekondari na Vyoo na ofisi katika shule ya msingi zote
za Kata ya Iyunbu wilayani humo moja ya mambo aliyoyasisitiza ni pamoja na
kufanyika Kwa vikao vya kikanuni.
Amesma vikao vya CCM vya Kata, Tawi na Mashina hufanyika kikanuni
kila baada ya miezi mitatu, ambapo vikao vya dharula hufanyika Wakati wowote
hivyo viongozi kukaa bila kufanya vikao ni Sawa na kuua Chama...
"mfano kata ya hapa Iyumbu hakuna kikao chochote
kilichofanyika Tangu kumalizika Kwa uchaguzi katikati ya mwaka 2022, hapo
kutakuwa na chama kweli,
Ni vizuri muitishe Vikao mkutane na wanachama kuanzia mashinani
na huko ndiko kwenye watu huko nawakikishia mtakutana na changamoto za wananchi
na itakuwa rahisi kuzitatua kuliko kuacha kila Mtu anaugulia maumivu yake
mwenyewe", amesema
Aidha amewanyooshea kidole wenyeviti wa mitaa ambao wanatokana
na Chama hicho kuwa na wao wanatakiwa kuitisha vikao ili kuchukua changamoto za
wananchi na kuzifanyia Kazi.
"Uongozi siyo utawara ni kuwatumikia wanachi ukiwaongoza
kwa kuwaonyesha njia na ndiyo maana waliwaamini na kuwachagua, katika Hili ni
vizuri pia kila mmoja ajitathini mwenyewe kama anatosha au laa ili asije
akikapa Kazi kubwa chama kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mitaa,
Unakuta mwenyekiti chama kinamuamini na kumpa nafasi lakini
baada ya kuchaguliwa anaanza kukidharau anakosa kukiheshimu na hata wengine
kukiwa na shuhuli za chama au vikao kama hivi hawaonekani, kama hapa iyumbu
ambapo kwa mitaa yote minne hakuna hata mmoja aliyeshiriki hii si dalili
nzuri", amesema
Kuhusu Changamoto zilizoibuliwa katika Kata hiyo ni pamoja na
ukosefu wa kivuko katika korongo linalotenga mitaa ya Udom na Nyerere kuliko na
shule za msingi na sekondari ambapo mvua zikinyesha mawasiliano hukatika
kutokana na maji kutwama, Wanachi pamoja na kulipia Aridh Kwa muda mrefu bado
hawajapatiwa Hati, fedha zaidi ya 600.Mil ambazo bado Kata haijalipwa na
kampuni ya ujenzi wa Reli ya mwendokasi kutokana na kuchimba na kuchukua kifusi
katika mlima uliyopo mtaa wa iyumbu, ukosefu wa maji katika sehemu ya mtaa wa
mwinyi pamoja na kutopimiwa mashamba Yao, vijana wakata hiyo kutonufaika na
ufundi au vibarua Kwa miradi mbalimbali ya ujenzi inayofanywa na taasisi mbalimbali.
Huku wanaccm wakiwataka viongozi wa CCM kukieneza chama hicho
bila kuangalia Ukubwa wa Ukoo, Familia, Umaarufu wala utajili Bali uangaliwe
uwezo wa mtu katika kuwaongoza na kuwasaidia wananchi
Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kuibua na kutatua changamoto
katika Kata hisika ambapo Mwenyekiti Mwanga aliambatana na mjumbe kamati ya utekelezaji
Raimond Magoda, Mjumbe Halimashauri ya Wilaya Samwel Kisaro na mjumbe wa kamati
ya utekelezaji toka jumuiya ya wazazi kwenga UWT,Ashura Kimwaga