CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kupitia vikao vyake vya juu leo Jumatano, Agosti 26, 2026, kimetangaza kumteua Deogratius John Ndejembi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akichukua nafasi iliyoachwa wazi baada ya kujiuzulu kwa Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi.
Ndejembi, ambaye kwa sasa anahudumu kama Waziri wa Nishati, anaingia katika nafasi hiyo akiwa mwanasiasa mwenye uzoefu wa zaidi ya muongo mmoja katika uongozi wa chama, Serikali na Bunge. Taarifa za Bunge zinaonyesha kuwa amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, ikiwemo Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kabla ya kuwa Waziri.
Aidha Chama cha mapinduzi Kimetangaza kumfuta uanacha aliyekuwa Makamu wa Rais Dkt Emmanuel Nchimbi Baada ya Kuthibitika kuwa Katiba ya chama hicho pamoja na kanuni zake zilikiukwa..
Ni katika Taarifa iliyosomwa Usiku huu na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Asha rose Migiro Mara baada ya Vikao Vilivyokaa Agosti 26,2026 Jijini Dsm
Tags
SIASA
