BANDA MEDIA BLOG

ASKOFU MKUU DKT. MAIMBO AFUNGUA RASMI UTULIVU WA MAASKOFU NA WAKE ZAO BIHARAMULO.


 Na Rev. Maiko Luoga  - Biharamulo.

Askofu Mkuu Kanisa Anglikana Tanzania, Dkt.Maimbo Mndolwa  Ameongoza Ibada ya Ufunguzi wa Utulivu wa Maaskofu na Wake zao Unaofanyika katika Dayosisi ya kanisa hilo ya Biharamulo, Mkoani Kagera huku akisisitiza maombi kwa kanisa na mshikamano kwa waumini

Ibada ya Ufunguzi, imefanyika  25 Agosti 2026 katika Ukumbi Mpya wa Hoteli ya Ebeneza, Dayosisi ya Biharamulo, (Ebenezer Conference Hall) na kuhudhuriwa na Maaskofu wa Dayosisi, Maaskofu Wateule kutoka Dayosisi za Kahama, Zanzibar na Handeni pamoja na wake zao.

“Tukiwa mahali hapa kwaajili ya Utulivu, Tuzidi kuliombea Kanisa letu Takatifu hapa Tanzania na Ulimwenguni kote lizidi kuwa Imara, Tuombee Dayosisi zetu na waumini ili umoja na mshikamano utawale” alisema Askofu Mkuu Maimbo.

Ratiba ya Utulivu wa Maaskofu na Wake zao, Imeandaliwa na Ofisi Kuu ya Kanisa Anglikana Tanzania kupitia Askofu Mkuu Maimbo Mndolwa, Itaendelea hadi siku ya Jumamosi Tarehe 29 Agosti 2026 itakapohitimishwa.

Aidha Ratiba hiyo Imehudhuriwa na wageni pamoja na wakufunzi kutoka nchini Uingereza ambao wanapata nafasi ya kuzungumza na maaskofu pamoja na wake zao wakijadili maendeleo ya Kanisa Anglikana Tanzania.  

     

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG