Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman ( kulia) akizungunza na Katibu Mtendaji wa Tasisi ya Mpango wa Hiari ya kujitathimini katika masuala ya Utawala Boara Afrika ( APRM), Bwana Lamau Mpolo huko ofisini kwa Makamu Migombani mjini ZANZIBAR leo tarehe 22 Agosti 2023. ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar)
Zanzibar
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman , amesema kwamba kuwepo kwa Taasisi ya
Kujitathmini kwa hiari Afrika katika
masuala ya Utawala Bora ni fursa muhimu ya kusaidia kukuza uchumi na maendeleo endelevu
nchini.
Mhe. Othman ameyasema hayo ofisini
kwake Migombani mjini Zanzibar alipokutana na kufanya mazungunzo na ujumbe wa
Taasisi hiyo kutoka Tanzania Bara uliongozwa na Katibu Mtendaji wake Bwana
Lamau Mpolo.
Mhe. Othman amesema kwamba taasisi
hiyo inapaswa kuelekeza juhudi zake kwa kuangalia kasoro na mapungufu kwenye masuala mbali mbali katika kuchangia kasi ya uwajibikaji ili
kuimarisha uchumi na kuiwezesha nchi kuondoka mahali ilipo sasa na kuweza
kusonga mbele kimaendeleo.
Amefahamisha kwamba masuala
yanayohusishwa na taasisi hiyo ya kujitathimini
katika suala la utawala bora yanagusa uwajibikaji
kwa viongozi na wananchi ni muhimu hasa kwa vile yanazingatia maeneo
yote ya kiuchumi na kimaendeleo kwa taifa na jamii kwa jumla .
Amesema katika kuunga mkono juhudi
hizo ni lazima taasisi hiyo kupewa umuhimu stahiki kutoka kwa jamii watendaji
na serikali kwa jumla ili iweze kuakisi vyema mahitaji na mipango bora ya
maendeleo kwa nchi kwa kuwa masuala hayo yanamchango mkubwa katika maendeleo ya
nchi.
Amesema kwamba iwapo masuala hayo
yatapewa umhimu unaostahiki inawezekana ndani ya Tanzania kuwepo matokeo chanya
ya kimaendeleo kwa taifa katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi na taifa kuweza kupiga hatua kama
ilivyofanyika katika nchi mbali mbali duniani.
Aidha amesema kwamba masuala hayo
yanapopewa msukumo stahiki pia yanachangia
kuimarisha mahakama zenye ufanisi mkubwa ambazo ni moja kati ya nyenzo
kubwa za kiuchumi na maendeleo.
Amefahamisha kwamba nchi mbali
mbali zenye mahakama zinazowajibikaji kwa ufanisi zimechangia sana mataifa hayo
kuweza kupiga hatua katika kukuza uwekezaji kwenye sekta na maeneo mbali
mbali na hivyo kuimarisha upatikanaji wa
mapato na kukuza uchumi wa nchi zao jambo ambalo linaweza kutumika pia kwa
Tanzania na ikaweza kupiga hatua.
Aidha Mhe. Othman amesema kwamba
iwapo masuala hayo yatasimamiwa ipasavyo
yatasaidia sana katika kurejesha imani kwa wananchi kwa kuwa viongozi pia watasiamia maadili na
kuitaka taasisi hiyo kuzitangaza kwa wananchi shughulizao mbali mbali wanazofanya ili kujenga uwelewa bora kwa umma.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa
Taasisi hiyo ya Mapngo wa hiari wa kujitathimini katika masuala ya utawalabora
na demokrasia Afrika nchini Tanzania Lamau Mpolo amesema kwamba Taasisi hiyo ni
muhimu na inaendelea na jitihada za uratibu katika dhana ya utawala bora kwa
kuonesha kasoro na kutoa mapendekezo juu ya namna ya kufanya marekebisho katika
maeneo mbali mbali.
Amesema kwamba hivi karibuni
taasisi hiyo itapita kwa wananchi katika maeneo mbali mbali ya Tanzania ili
kusikiliza maoni hasa katika vigezo vya siasa , uchumi na utawalabora ambavyo
ndivyo vinavyotumika katika tathimi wanazozifanya.
Taasisi ya Mpango wa hiari ya kujitathmini katika
masuala ya utawala bora na Demokrasia
Afrika tayari imeridhiwa na nchi
43 kati ya 54 za Afrika yenye madhumuni ya kukuza dhana ya utawala bora kwa
kuzingatia vigezo vya ustawi wa kiuchumi
kwa jamii, siasa , Demokrasia ili kuleta
maendeleo endelevu.
Mwisho.