AFCON 2023: Kitendawili kwa Nyota wa Kimataifa wa Kiafrika
Raha ya soka ni ndani ya dakika 90, lakini maandalizi
yake ndiyo mapigo ya mchezo huo.
Huku mashabiki wakijawa na matarajio kutokana na furaha
isiyozuilika itakayoletwa na msimu ujao wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON),
utakofanyika Januari 13 hadi Februari 11, 2024, tayari mivutano ya nje ya
uwanja imeanza kurindima.
Mashirikisho ya soka ya Kiafrika yamekuwa kwenye msuguano
na vilabu vya Ulaya tangu Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kutangaza ratiba
ya mashindano, ikiwa na mataifa 24 yaliyojiandaa kupambania kombe katika
viwanja sita katika miji mitano ya Côte d'Ivoire.
Vilabu vingi vya Uingereza vinaweza kupoteza wachezaji
wao maarufu wa Kiafrika ikiwa AFCON itafanyika katikati ya msimu, na karibu
vyote haviko tayari kuwaachilia wachezaji hao kabla ya tukio hilo.
Dk Patrice Mostepe, rais wa CAF, anasisitiza kuwa
mashindano hayo yalilazimika kusogezwa kutoka majira ya joto mwezi wa
Juni-Julai - yanayoshabihiana na mapumziko ya kimataifa - hadi Januari wakati
huu kwa sababu ya hali ya hewa nchini Côte d'Ivoire.
Nyota wa soka wa Kiafrika wanabeba jukumu muhimu katika vilabu vyao nje ya nchi. Picha: CAF
"Si vyema
kwa soka la Kiafrika ikiwa tunaweza kuandaa mashindano yanayoweza kufutwa; sio
jambo zuri kwa bara zima," Mostepe alisema katika mkutano na waandishi wa
habari huko Morocco wakati wa kutangaza ratiba.
Niran Adesanya,
mchambuzi na mwandaaji wa michezo wa Nigeria, haonyeshwi kushangazwa na hatua
za vilabu vya Ulaya.
"Januari
na Februari ni wakati muhimu katika kalenda ya soka. Vilabu vya Magharibi
vinarejea kutoka mapumziko ya kimataifa, na kawaida ni wakati bora wa
kuijimarisha" Adesanya anaiambia TRT Afrika.
Nyota wa soka wa Kiafrika wanabeba jukumu muhimu katika vilabu vyao nje ya nchi. Picha: CAF
Uchochezi wa moja kwa moja
Mwezi Novemba
2021, kocha wa Liverpool Jürgen Klopp alilazimika kutoa ufafanuzi baada ya
kuitaja AFCON kama "mashindano madogo barani Afrika" wakati wa
mkutano wa waandishi wa habari baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
"Mara
nyingi nimesikia kwamba hakuna mapumziko ya kimataifa hadi Machi. Januari, kuna
mashindano madogo barani Afrika," alisema.
Dhihaka ya
Klopp juu ya AFCON iliamsha hisia za hasira kwenye mitandao ya kijamii, na
angalau mwandishi mmoja wa Kiafrika kudai kocha huyo aombe msamaha wakati wa
mkutano mwingine.
Mjerumani huyo
alisema kauli yake ilichukuliwa vibaya, akifafanua kuwa alikuwa tu akionyesha
kuchukizwa kwake na kupoteza wachezaji muhimu kama Sadio Mane (Senegal),
Mohamed Salah (Misri), na Naby Keita (Guinea) katika mashindano wakati huo.
Mwezi Desemba
2021, wiki chache kabla ya msimu wa Januari 2022 wa mashindano hayo, Rais wa
Chama cha Vilabu vya Ulaya, Nasser al-Khelaifi alilalamika juu ya vilabu kupata
pigo kwa kutokana na mwingiliano wa kalenda.
Lakini wakati
CAF imejitahidi hapo awali, kusogeza mashindano kwa miezi ambayo hali ya hewa
sio rafiki kwa soka.
Mafunzo ya Zamani
Katika AFCON
2019, iliyofanyika nchini Misri kati ya Juni na Julai, joto la jua lilikuwa
kubwa kiasi kwamba mchezaji wa Uganda Denis Onyango alilazimika kuondolewa
uwanjani wakati wa mechi. Mchezaji mwingine alidondoka mazoezini kutokana na
kuishiwa maji mwilini.
Ubora wa
mashindano hayo haukupata sifa kubwa pia, huku wachambuzi wakitaja kiwango
kikubwa cha joto la lilirekodiwa duniani kote wakati huo, hasa maeneo yenye
asili ya jangwa, lilidhoofisha uwezo wa wachezaji wakati wa mechi nyingi.
CAF inasisitiza
kuwa Januari ni wakati bora wa mwaka kwenye bara hilo kucheza mchezo mzito kama
soka. Imekataa kusogea licha ya malalamiko kutoka kwa vilabu vya Ulaya.
"Hapa
ndipo wachezaji wanavyochanganyikiwa, hasa wale ambao bado wanachipukia,"
anasema John Ofori, mchambuzi wa michezo wa Ghana.
"Lakini,
kwa bahati mbaya, wanapaswa kuchagua upande. Kucheza kwenye vilabu hivyo ambapo
wanavyojipatia kipato na kujenga fani yao. Mara nyingi wachezaji wanajikuta
katika nafasi ngumu ya utii."
Mwandaaji wa
kipindi cha michezo ya runinga wa Nigeria, Blessing Nwosu anakubaliana.
"Hili ni suala kubwa kwa sababu, kama vilabu vya Ulaya vinavyolalamika
kwamba wanahitaji wachezaji wao nyota ili kufanya vizuri katika mashindano,
vilabu vya Kiafrika pia vinahitaji wachezaji wao nyota kwa kampeni kubwa kama
AFCON."
CAF ilifikia
makubaliano ya dakika za mwisho na vilabu vya Ulaya kwa AFCON 2022 kuwaachilia
wachezaji hadi Januari 3. Ofori anasema makubaliano kama hayo ni kinyume cha
uzalendo.
"Ikiwa
mashindano ni karibu wiki moja kabla, makocha wanaweza kufanya nini kwa muda
mfupi huo? Wachezaji wanaweza kujenga uhusiano wa timu vipi? Wanapata muda gani
wa kutengeneza mkakati? Na maana yake ni kuwa sio haki kabisa. Vilabu vya Ulaya
vinapaswa kuheshimu mashindano haya zaidi," Ofori anaieleza TRT Afrika.
Vilabu vya
Ulaya vimeeleza kwamba wasiwasi wao wa kuwaachilia wachezaji unatokana na hofu
ya wachezaji hao kupata majeraha wakati wa AFCON, na hivyo hawataweza kufanya
vizuri kwa muda mwingine wa msimu.
Vilabu hivyo
pia wanasisitiza kwamba wachezaji wanaoachiliwa wanapata mishahara yao na
marupurupu wakati wanacheza kwa nchi zao. Kutokana na sababu hizo ni kwamba
vilabu vinastahili kufanya maamuzi makubwa zaidi.
Sheria zinazoegemea Vilabu
Sheria za FIFA
hazijasaidia kampeni za timu za soka za Kiafrika. "Vilabu wanapaswa
kuwaachilia wachezaji wao waliosajiliwa kwenye timu za kitaifa ambazo mchezaji
anastahiki kucheza kulingana na uraia wake ikiwa wito unatoka kwa shirikisho
husika," kulingana na kifungu Fulani cha Kanuni.
Lakini sio
lazima kwa vilabu kuwaachilia wachezaji nje ya dirisha maalum la kimataifa -
hakuna dirisha la Januari - na kwa mashindano makubwa ya kimataifa ya wachezaji
wakubwa zaidi ya moja kwa mwaka.
"Ni kama
kujaribu kupandisha jiwe kubwa juu ya kilima na viashiria vyote vikiwa kinyume
na wewe. Sheria hizo zinapaswa kuifanya iwe lazima kwa vilabu vya Ulaya
kuwaachilia wachezaji na kufanya hivyo kwa wakati. Kuifanya kuwa lazima ni sawa
na kuomba maamuzi yafanyike kama kibali," anasema Ofori.
Sasa basi,
wachezaji wa Kiafrika waliokwama katika hili wanaweza kufanya nini?
"Inategemea
sana wachezaji kusimama kidete," anasema Adesanya. "Wachezaji wengi
wa Kiafrika wameonyesha njia. Didier Drogba, Michael Essien na Samuel Eto'o,
kwa kutaja wachache. Wote waliiambia vilabu vyao, 'Hapana, nitacheza
AFCON.'"
Nguvu ya Fedha
Mwezi Agosti
2022, Rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis alitangaza kwamba klabu yake
haitasaini wachezaji wa Kiafrika isipokuwa wakubaliane kutoshiriki katika
AFCON.
Mchezaji wa
zamani wa Napoli na Msenegali, Kalidou Koulibaly alikosoa haraka tishio la De
Laurentiis, akisema linaweka wachezaji wachanga, wenye vipaji vya Kiafrika
wenye njaa ya kujenga kazi na kuishi nje ya nchi, kwenye nafasi ngumu.
"Kwangu
mimi, jambo muhimu zaidi ni kuheshimu kila mtu. Huwezi kusema juu ya timu za
kitaifa za Kiafrika kwa njia hii. Lazima uwaheshimu, kama vile unavyowaheshimu
timu za kitaifa za Ulaya."
Kampeni ya Nigeria katika AFCON 2023 inategemea sana ushiriki wa Osimhen. Picha: CAF
Mwanasoka wa Cameroon Eto'o pia alilizungumzia kwa uziyto
juu ya suala hilo, akisisitiza kwamba dunia inapaswa kubadilika na ratiba ya
mashindano ya kimataifa ya Kiafrika na wachezaji wa Kiafrika lazima wawe kitu
kimoja katika utetezi wa AFCON.
Kukosekana kwa mshambuliaji wa Napoli na Nigeria, Victor
Osimhen katika michezo ya awali ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 kulikuwa na
athari kubwa, na nafasi za Super Eagles kushiriki katika mashindano sasa ziko
hatarini.
"Napoli itaweka ugumu kumwachilia Osimhen kwa sababu
hawataki ajaribu jeraha kubwa lingine ambalo litamfanya awe nje ya uwanja kwa
wiki na kukosa michezo muhimu baada ya AFCON. Lakini basi, fikiria AFCON bila
Osimhen kwa mashabiki wa soka wa Nigeria," anasema Nwosu.
Huku mjadala ukiendelea, mashabiki wanaweza tu kutumai
kwamba mvutano huu utapata ufumbuzi.
“Sisi tunachotaka ni kwa bara letu kufurahia mchezo wa
soka. Tumekupitia changamoto nyingi za kimwili na kiakili. Kama wanadamu
nadhani tunastahili kusisimuliwa na furaha itokanayo na mashindano haya”
anamalizia Ofori.



