BANDA MEDIA BLOG

No title

 

Muuaji wa Beatrice James Akamatwa akutwa Amekunywa Simu Akitaka kujiua, Awahiwa

                      Beatrice James Minja Enzi za Uhia wake
                       ...................................................................

Jeshi la Polisi nchini limesema kuwa limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa mauaji ya Beatrice James Minja ambayo aliyafanya huko Tarekea Wilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjro Tarehe 12.11.2023 na mtuhumiwa aliyefanya aliyefanya tukio hilo kukimbia.

Akitoa taarifa hiyo leo  Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP David Misime amesema kuwa baada ya taarifa hizo kufika Jeshi la Polisi lilianza mara moja uchunguzi kumtafuta aliyefanya tukio hilo ambapo mapema leo Disemba 31.12.2023 Jeshi hilo lilifanikiwa kumkamata Mtuhumiwa Lukas Paul Tarimo.

 “jitihada zilizoanza toka tarehe 12 Novemba 2023 liliporipotiwa tukio la Beatrice James Minja kuchomwa visu na hatimaye kufariki tarehe 27 Disemba 2023 katika Hospital ya KCMC zimezaa matunda.”

SACP Misime amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa mafichoni huko Kijiji cha Jema kata ya Olondonyosambu Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha.

Aidha amebainisha kuwa baada ya Mtuhumiwa kuhisi atafikiwa na Mkono wa sheria alijaribu kunywa sumu ya kuua wadudu lakini Jeshi hilo lilifanikiwa kuwahi sehemu alipo mtuhumiwa huyo na jitihada za kumkimbiza katika kituo cha afya zilifanyika ambapo alipata matibabu na anaendelea vizuri huku akisubili taratibu za kisheria.

Pia Msemaj wa Jeshi hilo amewashukuru wananchi kwa ushirikiano wao na Jeshi la Polisi kitendo kilichopelekea mtuhumiwa wa mauaji kukamatwa huku akiwaomba wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo.

“Tunawashukuru sana wananchi wa kata hiyo kwa ushirikiano mkubwa waliotoa kwa Jeshi la Polisi hadi kufanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ingawa baada ya kuhisi mkono wa serikali unakaribia kumfikia alikunywa sumu inayotumika kuua wadudu, mtuhumiwa amepatiwa huduma ya kwanza yupo vizuri na taratibu za kisheria zinaendelea,” amesema.

Juzi Ijumaa Jeshi la Polisi lilijitokeza na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano wa taarifa kwa jeshi hilo ili kubaini alipo kisha kumkamata mtuhumiwa Lucas Tarimo.

Tarimo anadaiwa kumchoma visu na kumsababishia umauti Beatrice James Minja mkazi wa Rombo mkoani Kilimanjaro ambaye alikuwa na mahusiano naye ya kimapenzi kabla ya wawili hao kuachana.

Hata hivyo, mtuhumiwa huyo alikuwa anadaiwa kuwa msaidizi wa mashamba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda na mbunge wa Rombo lakini kiongozi huyo alikana kumfahamu ‘shamba boy’ huyo.

Hatua hiyo ilikuja saa chache baada mwanaharakati wa masuala ya mitandaoni, Godlisten Malisa kuchapisha kwenye akaunti yake ya Instagram taarifa ya mwanamke huyo aliyedaiwa kushambuliwa kwa visu 25 na Paul Tarimo aliyedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Beatrice.



Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG