BANDA MEDIA BLOG

No title

RC HADIDI AWATAKA WANANCHI KUKIMBILIA FURSA ZILIZOPO KASKAZINI

Msaidzi mkurugenzi wakala wa  uwekezaji ZIPA Saleh sani akizungumzia fursa zinazopatikana za uwekezaji katika mkoa wa Kaskazini Unguja wakati wa majadiliano yaliyoangazia  fursa na mbinu za kuzifikia uliofanyika ukumbi wa Mitihani Bumbwini Kaskazini “B”.
Mkurugenzi wa habari na matukio Shirika la utangazaji  Zanzibar ZBC Salum Ramadhan akizungumza machache na kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini unguja Rashid Hadid Rashid  kuzungumzia fursa zinazopatikana katika Mkoa huo,huko ukumbi wa Mitihani Bumbwini Kaskazini “B” Unguja.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Rashid Hadid Rashid akizungumzia fursa zinazopatikana katika Mkoa huo huko ukumbi wa Mitihani Bumbwini Kaskazini “B” Unguja.

Mkurugenzi mafunzo wakala wa uwezeshaji wananchi kiuchumi  (ZEEA)Fatma Mohammed  Juma akizungumzia fursa zinazopatikana za uwezeshaji wananchi kiuchumi katika mkoa wa Kaskazini Unguja wakati wakati wa majadiliano yaliyoangazia  fursa na mbinu za kuzifikia yaliofanyika ukumbi wa Mitihani Bumbwini Kaskazini “B”.
Baadhi ya wajumbe  wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa kaskazini unguja wakiwa katika hafla ya majadiliano yalioangazia fursa zinazopatikana katika mkoa huo na mbinu za kuzifikia yaliyofanyika  ukumbi wa Mitihani Bumbwini Kaskazini “B”.
Baadhi ya viongozi wa chama na Serikali pamoja na wananchi wa Mkoa wa kaskazini unguja wakifuatilia majadiliano yaliyoangazia fursa zinazopatikana katika mkoa huo na mbinu za kuzifikia huko  ukumbi wa Mitihani Bumbwini Kaskazini “B”.

 Ashura Muhammed Haji kutoka baraza la vijana Kaskazini unguja akichangia wakati wa majadiliano yalioangazia  fursa za mkoa wa kaskazini unguja    na namna ya kuzifiki, huko  ukumbi wa Mitihani Bumbwini Kaskazini “B”.

PICHA NA FAUZIA MUSSA- MAELEZO ZANZIBAR

NA RAHMA KHAMIS,     MAELEZO

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Rashid Hadid Rashid amewataka Vijana kuzikimbilia fursa zinazopatikana ndani ya Mkoa huo ili kujiendeleza kiuchumi.

Akizungumza wakati wa  mjadala ulioangazia kuzielezea fursa za mkoa huo na namna ya kuzifikia huko ukumbi wa mitihani  Bumbwini amesema fursa ni kitu muhimu kwa vijana kwani inawawezesha kujikimu katika maisha yao ya kila siku.

Amesema Mkoa wa Kaskazini una fursa nyingi ikiwemo Utalii, Kilimo, Afya na Elimu hivyo ni wajibu kwa kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika fursa hizo ili kunufaika nazo.

“Mkoa wetu umebarikiwa fursa nyingi za kuwainua wananchi hatuna budi kuzitumia fursa hizi ili kujikomboa na hali ngumu ya maisha” alissisitiza Hadid.

Aidha amefahamisha kuwa katika kuwajengea uwezo vijana, Serikali imejenga  masoko saba katika maeneo mabali mbali ndani ya Mkoa huo ili kuwawezsha vijana kupata fursa za ajira hivyo ni wajibu wao kujipanga na kuzitumia fursa hizo kwa lengo la kufaidika.

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha vijana wanazitumia fursa hizo ipasavyo zaidi ya vijana elfu moja tayari wameshapatiwa mikopo ili kujiwezesha kiuchumi.

Nae Msaidizi Mkurugenzi Mamlaka ya Uwekezaji (ZIPA) Saleh Said amesema miongoni mwa majukumu ya ZIPA ni kusajili miradi yote iliyopo katika Mkoa na kuweka viwango vya uwekezaji kwa wageni 

Ameongeza kuwa katika kuwapatia fursa wawekezaji wa ndani mamlaka imeweka unafuu kwa  wawekezaji wa ndani ukilinganisha na wageni ambao wahitajika kulipa zaidi ya dola millioni mbili.

Wakitoa ushauri wao wananchi wa Mkoa wa Kaskazin Unguja wamewaomba mamlaka husika kuwapatia elimu ya miradi inayojengwa pamoja na kuwekewa maafisa katika kila Wilaya ili waweze kupata mikopo kwa urahisi na kuondoa usumbufu wanapohitaji mikopo hiyo.

Majadiliano hayo ni mwendelezo wa Kampeni ya mkono kwa mkono kuelekea  maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG