BANDA MEDIA BLOG

No title

 

WIZARA YA ELIMU KWA KUSHIRIKIANA NA KOICA YAZINDUA MAABARA ZA KISASA

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar Lela Muhammed Mussapamoja  na viongozi mbalimbali wakitembelea miongoni mwa maabara zilizojengwa na shirika la Koica ikiwa ni  utekelezaji wa mradi wa kuimarisha elimu ya Sekondari Zanzibar,huko Machui Mkoa wa kusini  Unguja. (PICHA NA MPIGA PICHA WETU)

…….

Na Imani Mtumwa ,    Maelezo

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe,Lela Mohammed Mussa amesema Serikali itaendelea kushirikiana na mashirika mbalimbali katika  kuimarisha maendeleo ya kielimu Nchini.

Akizungumza katika makabidhiano ya maabara  za kisasa zilizojengwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Huduma za Miradi, kwa ushirikiano wa Korea (KOICA)  huko Skuli ya Sekondari Machui Wilaya ya Kati Unguja amesema makabidhiano hayo ni  utekelezaji wa mradi wa kuimarisha elimu ya Sekondari Zanzibar.

Aidha amesema Shirika la KOICA ni moja kati ya Shirika linalo unga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuboresha Miundo mbinu mbali mbali hasa katika sekta ya Elimu.

Hata hivyo amesema Wizara itasimamia kwa karibu ili  kuhakikisha Vifaa vya Maabara  vinapatikana kwa Awamu na kutuzwa vizuri kwa matumizi ya Maabara hizo.

Vile vile ameeleza, kuwepo kwa Maabara  za kisasa Unguja na Pemba kutasaidia wanafunzi kusoma vizuri kwa vitendo na kuleta matokeo chanja katika masomo ya Sayansi.

Aidha aliwataka wazazi wa eneo hilo kujua majukumu na wajibu kwa watoto wao na kuhakikisha Wanafunzi wanasoma vizuri ili kuweza kuendeleza elimu Nchini.

 Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Khamis Abdullah Said amelishukuru Shirika la Koica  kwa kuwapatia  uwezo Walimu zaidi 1300 katika  ufundishaji wa  masomo ya Sayansi.

Aidha, amewataka wanafunzi kuzitumia vyema Maabara hizo pamoja na kusoma kwa bidii ili kufikia lengo lililokusudiwa .

Akisoma Risala  Mkurugenzi wa Koica nchini Tanzania Bw. Jieun Seong  amesema Mradi huo wa kuboresha Maabara za kisasa umeanza Mwezi  January 2020 na kumalizika Mwezi wa Septemba  2023.

 Amesema  Jumla ya shiling Milioni 3 USD Dolar, zimetumika mpaka kukamilika kwa Mradi huo wenye lengo la  kuboresha Sekta ya Elimu katika nyanja ya Masomo ya Sayansi

  Amesema, Jumla  ya Maabara zilizo jengwa ni kumi kwa Unguja na Pemba. ikiwemo  Bubwini, Fukuchani, Jendele, Machui, na Jongowe Sekondari Skuli kwa Unguja na   Chambani, Chanjamjawiri, Shumba, Uondwe na Wambaa kwa Upande wa Pemba.

Nao baadhi ya wazazi na walezi wamesema wataungana pamoja  na Serikali kwa kutoa ushirikiano wao ili kuhakikisha watoto wao wanasoma na kuvitumia vifaa vya maabara hiyo ili kukuza sekta ya elimu katika jamii.


Katibu Mkuu Wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Khamis Abdalla Said (katikati), naibu Mkurugenzi KOICA Tanzania Jieun Seong (kushoto) na meneja mradi wa UNOPS John. Bundu Fofanah (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja  katika hafla ya makabidhiano ya maabara za kisasa na vifaa baina  ya Wizara ya elimu na Serikali ya jamuhuri ya korea kupitia shirika la Koica huko  skuli ya Machui Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni  utekelezaji wa mradi wa kuimarisha elimu ya Sekondari Zanzibar.


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar Lela Muhammed Mussa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha maabara  skuli ya Machui  ikiwa ni  utekelezaji wa mradi wa kuimarisha elimu ya Sekondari Zanzibar kilichojengwa na wazazi  kwa kushirikiana Koica .

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG