Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Asia Juma akimlisha kipande cha Keki Mmoja wa watu wasioona ambao nao walipata fursa ya Kupata afunzo hayo ya Ujasiriamali
MJUMBE wa Baraza Kuu la Taifa la chama cha
Mapinduzi CCM Asia Juma amesema Chama cha CHADEMA ni sawa na Mtoto wa Mwisho
ambaye huwa haaichi kualamika na kuanzisha visa na wakati mwingine mikasa ili
mradi asikike na kusaidiwa.
Ameayasema hayo wakati alipokuwa akifunga mafunzo
ya Ujasiliamali yalitofanyika kwa wiki moja katika kata ya Nkuhungu jijini
Dodoma yaliyowajumuisha wakazi zaidi ya 150 wa kata hiyo.
Asia aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo
kutojihusisha na Maandamano yaliyoitishwa na Chama cha CHADEMA badara yake
wakatengeneze, Biskuti, Batiki, Keki, Clpis, Karanga za Kusaga na bidhaa
nyingine nyingi walizofundishwa Wakauze ili kuendelea kulea familia zao
“chadema ni kama kitinda mimba, kitinda mimba mara
zote huwa hajiamini katika familia ndiyo maana huwa haishi kijilalamisha hata
kwa mambo yasiyo ya msingi, malengo yake huwa anahitaji kusaidiwa ni mtu kudeka tu,
Huwezi kuendesha Nchi kwa kumdekeza kitinda mimba ambaye kazi yake ni kujidekeza
kwenye miguu ya mama yake, we ona Miswada yote ambayo wadau mbalimbali mpaka
CHADEMA wenyewe waliyachangia maoni, lakini kabla hayajafika popote, tayari
wametoka na kuanza kujilalamisha na kuwashawishi Watanzania waingie Barabarani
kwa ajili ya maandamno kwani walijibiwa kuwa maoni hayafanyiwi kazi? Alisema na
kuhoji.
Asia ambaye Pia ni Mjumbe wa Baraza kuu la UWT
Taifa na mjumbe wa mkutano mkuu wa Mkoa wa Dodoma kupitia Wazazi amesema pia Kwenye
Maandano huwa hamna ustaarabu wowote mtu anweza kushiriki kisha akaumia ingekuwa
bora waachiwe viongozi kina MBOWE wenyewe na familia zao wakaandamane.
Hivi karibuni chama cha CHADEMA kupitia mwenyekiti wake Ffreeman Mbowe kilitangaza maandamano ya Amani Bila kikomo Nchi Nzima, hadi Pale, Serikali Itakapofanyia kazi Maoni na Mapendekezo ya Wadau kuhusu upatikanaji wa Katiba Mpya na Chaguzi huru na Haki, ambapo alisema maandamano hayo yanatarajiwa kuanza siku ya Jumatano ya Tarehe 24 mwezi huu.