BANDA MEDIA BLOG

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA SHERIA NA KATIBA YAWASHANGAA VIONGOZI WA CHADEMA


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Joseph Mhagama akifafanua jambo wakati alipokuwa akiongoza kikao cha kamati hiyo leo Bungeni Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Joseph Mhagama, akiongea Na Vyombo vya Habari katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma leo januari 22,2024

          ...........................................................

                        Na John Banda, Dodoma

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Sheria na Katiba, imesema Imeshangazwa na Chama kimoja kati ya vyama 13 Vilivyoshiriki katika utoaji wa Maoni ya Miswada ya Sheria ya Uchaguzi uliofanyika hivi karibuni jijini Dodoma kwa kutoka hadharani na kutangaza maandamano kwa ajili ya  kile alichoita kutaka kudhoofisha mchakato unaoendelea.

Hivi karibuni chama cha CHADEMA kupitia mwenyekiti wake  Ffreeman Mbowe kilitangaza maandamano ya Amani Bila kikomo Nchi Nzima, hadi Pale, Serikali Itakapofanyia kazi Maoni na Mapendekezo ya Wadau kuhusu upatikanaji wa Katiba Mpya na Chaguzi huru na Haki, ambapo alisema maandamano hayo yanatarajiwa kuanza siku ya Jumatano ya Tarehe 24 mwezi huu.

Akiongea na Waandishi ya Habari kando ya Kikao cha Kamati hiyo kilichokuwa Kikiendelea Leo Januari 22,2024 Bungeni Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Joseph Mhagama amesema alitegemea viongozi wakuu wa Chedema kwa kuwa walishawahi kuwa wabunge na wanajua utaratibu wangewaelekeza wananchi kuhusu hatua muhimu zinazoendelea baada ya maoni kutolewa.

Mhangama amesema kamati hiyo ilipokea maoni yote ya wadaua na kutengenezea jedwari kisha wakayapeleka Serikalini..

“baada ya kamati yangu kuyapokea maoni ya wadau imeshakaa na kuyachambua kisha imetengeneza jedwari na kulipeleka serikalini, kinachosubiliwa kwa sasa ni serikali kuja kwenye kamati kwa ajili ya majadiliano na makubaliano”, amesema

Ameongeza kuwa baada ya taratibu za kamati ya kudumu ya Bunge na serikali kukamilika kisha kukawa na baadhi ya vifungu havijakaa sawa serikali itatengeza Jedwari ambalo litapelekwa Bungeni kwa wawakilishi wa wananchi nao watapitia na litajadili kifungu kwa kifungu kipi kipite kipi kisipite.

Amesema Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Katibu mkuu wa Chama hicho Tundu Lisu na Naibu Katibu Mkuu,  John Mnyika wao wameshwahi kuwa Wabunge na utaratibu huo wanaujua ila wanachokifanya kuitisha Maandamano hayo  ni kutaka kuwavuruga watanzania na kulivuruga Bunge lisitekeleze wajibu wake wa Kikatiba.

“kwa maana hiyo hawa wenzetu wanataka kudharau maoni yote yaliyotolewa na wadau pamoja na watanzania wote kwa ujumla”, amesema

Mhe. Mhagama amebainisha kuwa katika siku 4 za kusikiliza na kukusanya maoni ya Wadau na watanzania Kamati hiyo ilishuhudia idadi kubwa ya Uwakilishi kutoka katika makundi mbalimbali yakiwemo Taasisi za Dini, Taasisi za kiraia, Vyama vya Siasa na wananchi wa kawaida idadi ikiwa 1,707 ambayo ni kubwa kuwahi kutokea katika utoaji wa maoni hapa nchini.  








 

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG