BANDA MEDIA BLOG

KATIBU MKUU WACCM DK. NCHIMBI AKARIBISHWA DODOMA AWATAKA WANACCM KUJITOFAUTISHA

 














NA, JOHN BANDA, DODOMA

KATIBU Mkuu wa CHAMA cha Mapinduzi CCM Balozi Dkt,Emanuel Nchimbi amesema kuwa kama Chama watakuwa mstari wa mbele kutaka maridhiano na Vyama pinzani huku akiwataka wanaCCM kubishana na Vyama vya upinzani  kwa hoja kwakujitofautisha kutokana na ukongwe Wake.

 Ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati alipokuwa akipokelewa katika viwanya vya CCM, Makao Makuu jijini Dodoma. 

 Dkt, Nchimbi amesema kila mwana chama anatakiwa kujua umuhimu wake  ndani ya chama kuanzia ngazi za mashina hadi taifa.

 " Tukumbuke kuwa chama ni wana chama na ndio maana kazi ya kukitangaza ni ya wanachama wenyewe, "Amesema Dkt Nchimbi

 " Niwaombe Sana waana CCM kakitangazeni chama  kwa ni hakuna mwenye uchungu na chama chake kama mwanachama mwenyewe chukueni dhima hiyo Kutakana kukitangazani chama kwa hoja nasio kwa ushabiki kitofautisheni chama kikongwe hivi vyama vinavyochipukia, "Amesema Dkt Nchimbi

 Aidha amewataka wanachama wote kuanzia ngazi ya Shina  kuhakikisha wanakitetea na kukisemea Chama vizuri kutokana na mambo mazuri yanayofanywa na chama hicho

Kwa upande Wake,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,ROSEMARY SENYAMULE amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na uchapa kazi Wake huku akishukuru kwa miradi ya kimkakati inayotekekezwa Dodoma ikiwemo ujenzi wa Standard gauge.

 Awali  Aliekuwa Mbunge wa CHADEMA  Viti maalum,Upendo Peneza ambaye amehamia CCM  amemsifia Rais Samia SULUHU Hassan kuwa ni mwanamageuzi  wa kweli katika kusimamamia haki na Demokrasia ya nchi huku akiahidi kutoa ushirikiano kwa CHAMA katika kuleta maendeleo

 Hata hivyo Pendeza Amesema ameamua kuhamia CCM, kutokana na Rais Samia kuweka mazingira Mazuri kwa vyama vya Siasa, wadau na wananchi kwa ujumla kuhusu kuweka mazingira ya Umoja wa kitaifa kwa kukubali kukaaa pamoja kwa ajili ya Maridhiano. 

Kada huyo Mpya wa CCM, aliyehama Chadema ambako aliwahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum na mwenzake aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Manyara, Benson Andrew pamoja na Onesmo Mbuya katibi wa CHADEMA wilayani Morogoro... 


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG