Waziri wa Fedha wa Kenya Njuguna Ndung'u / Picha: Reuters
Benki ya Biashara na Maendeleo (TDB) imeikopesha Kenya kiasi cha dola milioni 210, Waziri wa Fedha wa nchi hiyo Njuguna Ndung'u ameiambia Reuters, kabla ya muda wa kukomaa kwa EuroBond yenye thamani ya dola bilioni 2 mwezi June, mwaka huu.
Kushuka kwa akiba ya fedha za kigeni, kushuka kwa thamani ya shilingi ya Kenya na changamoto za mapato zimeibua maswali kuhusu uwezo wa Kenya wa kulipa Eurobond, ingawa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF imesema haitegemei kwama Kenya itashindwa kulipa.
Mkopo huo wa TDB, benki ya maendeleo ya Kiafrika inayohudumia nchi wanachama 25, ni sehemu ya mpango wake unaotakiwa kutoa kiasi cha dola bilioni 1 katika mpango wa usimamizi wa Kenya, amesema Ngung'u.
Amesema, Kenya inapaswa kupokea kiasi cha dola milioni 500, lakini benki imewasilisha kiasi cha dola milioni 210 pekee.
Ndung'u hakusema ni kwa namna gani mkopo huo utatumika. Gavana wa Benk Kuu ya Kenya alisema mwezi Disemba mwaka jana kuwa TDB ingeikopesha Kenya dola milioni 300 ambazo zingetumika kununua sehemu ya Eurobond.
Bodi ya utendaji ya IMF katikati mwa juma, imepitisha mkopo wa dola milioni 941 kwa Kenya, kutoa ahueni ya kifedha.
