BANDA MEDIA BLOG

Mo Salah wa Misri kukosa michuano ya AFCON

 

Mohamed Salah / Picha: Maktaba AFP / Photo: AFP Archive

"Vipimo vya X-ray alivyofanya Salah vimethibitisha kwamba ana jeraha la mkononi na kwamba atakosa kuchezea timu yake katika mechi mbili katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Cape Verde na raundi ya 16 iwapo (Misri) itafuzu," imesema taarifa fupi ya EFA.

Mapema Ijumaa, daktari Mohamed Abu El-Ela wa Misri alisema, Salah awali alitaka kuendelea kucheza katika michuano muhimu lakini maumivu yalipozidi aliomba kuondolewa. 

Ukubwa wa jeraha

Meneja wa Salah wa Liverpool, Juergen Klopp, alisema mapema kwamba jeraha hilo linaweza kuwa kubwa, akisema mchezaji huyo ni nadra kuumizwa au kutoka mchezoni anapokuwa uwanjani.

"Nimezungumza nae jana usiku. Wanafanya vipimo zaidi na baadae tutajua zaidi," Klopp aliwaambia waandishi.

 


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG