NAIBU Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amemtaka Mkandarasi wa Mradi wa Maji wa Miji 28 kuongeza kasi na nguvu ya utekelezaji wa mradi huo ili wananchi wapate maji haraka na kuondokana na adha ya ukosefu wa maji.
Mhandisi Mahundi ametoa agizo hilo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maji jana Januari 23 2024, Urambo Mkoani Tabora ambapo ametembelea mradi wa maji wa miji 28 ikiwemo kijiji cha Ndono ambapo bomba la kupeleka maji Urambo linapojengwa.
Aidha Mhandisi Mahundi amewahakikishia wana Urambo kuwa ifikapo mwezi Oktoba 2025 wananchi wa Urambo watakunywa
Maji safi na salama yatokanayo na mradi huo wa maji wa miji 28 unaotoa maji kutoka ziwa Victoria utakaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 145.
” Wananchi hawa wa Urambo watanufaika na maji kutoka katika bwawa la Kalemela linalojengwa lenye thamani ya shilingi Bilioni 5 na niwahakikishie mpaka ifikapo mwezi Oktoba changamoto ya maji hautakuwepo eneo hili”amesema Mhandisi Mahundi
