> _Akemea tabia ya baadhi ya Askari Polisi kuchukua rushwa_ .
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda ametoa maelekezo ya CCM kwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang Ndugu. Janeth Mayanja kuhakikisha haki inapatikana kwa Mwananchi nwenye mgogoro wa mpaka wa ardhi baina yake na Polisi katika Mji mdogo wa Katesh Wilayani Hanang.
Mwananchi huyo alitoa malalamiko yake mbele ya Mwenezi Makonda aliposimama kusalimiana na Wananchi wa eneo la Katesh ambapo alibainisha kupokonywa bango na polisi alilondika kero yake Pamoja na kuvunjiwa nyumba yake kutokana na kuonekana kutoa taarifa ya baadhi ya Askari kukamata wanywa gongo na kuomba kupewa hongo ya Tsh 700,000/=.
Mara baad ya kusikiliza malalamiko hayo, Mwenezi Makonda alibaini kuwa kutokana na Mwanachi huyo kutoa taarifa ya askari kutaka rushwa ndio imepelekea Askari hao kwa kushirikiana na watu wa Ardhi Halmashauri ya Hanang kwenda kuvunja nyumba ya Mwananchi na angali Mwananchi huyo ameeleza kuwa kesi ya mgogoro wa mipaka baina yake na eneo la polisi ilishafutwa mahakamani kutokana na kukosekana kwa ushahidi ya kuwa ni eneo la polisi mahali alipojenga nyumba yake na nyaraka za mahakama anazo.
Baada ya hayo, ndipo Mwenezi Makonsa akatoa maagizo ya CCM ya kumtaka Mkuu wa Wilaya kukaa na OCD na Mwananchi huyo kwa kushirikisha anapewa haki zake.
Vilevile amemtaka DC Hanang kuhakikisha yaliyosemwa na mzee huyo kuhusiana na askari kutaka rushwa kama yakithibitika basi hatua za kisheria na kinidhamu zichukuliwa kwa Askari hao.
📍 Mji mdogo wa Katesh
