BANDA MEDIA BLOG

MWENEZI CCM, AMUAGIZA MKURUGENZI KULIPA 27.5 ZA VIJANA MAFUNDI


MKuu wa Mkoa wa Manyara Ndugu. Queen Sendiga amemuagiza Mkurugenzi wa Hanang Ndugu. Francis Namauombo kwa kumpa siku 5 kulipa deni la  Tsh Milioni 27.5 kwa Vijana waliofanya kazi kutengeneza madirisha ya shule.

" *Vijana wana haki kwa namna nilivyosikiliza vema malalamiko na majibu ya Mkurugenzi wetu hivyo naomba nikuhakikishie Ndugu Mwenezi Makonda kama serikali ilifanya ubovu wa kusainj hati mbovu na ubovu huohuo wautumie kuwalipa pesa zao Vijana hawa na namuagiza hapa Mkurugenzi huyo wa Hanang kuhakikisha ndani ya siku 5 hadi kufikia Januari 30 pesa hizo zote Milioni 27.5 ziwe zimelipwa kw Vijana hao* " Alisema RC Sendiga

Hatua hiyo.imekuja mara baada ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda kutoa maelekezo ya CCM kwa Mkuu wa Mkoa kuhakikisha kikundi cha Vijana wanaodai fedha zao kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Hanang. Ndugu. Francis E. Namaumbo zinalipwa.

Mmoja kati ya Wananchi wa Hanang alisema malalamiko hayo kwa Mwenezi Makonda aliposimama kuwasalimia Wananchi wa Mji mdogo wa Katesh akiwa njiani kuelekea Mkoani Singida leo tarehe 25 Januari, 2024.

Mwananchi huyo ameeleza kuwa walifanya kazi ya kutengeneza madirisha ya shule yenye thamani ya Tsh Milioni 27.5 na angali tayari mhandisi wa Wilaya alishawapatia hati ya kuonesha kumalizika kwa kazi tangu mwezi Septemba, 2023 na bado hawakilipwa na baada ya kusikikia kwa ujio wake ndio akaitwa na kupelekwa site kisha akaambiwa hakuna ubora wa kazi aliyoifanya na kudai wamlipe Tsh Milioni 13.5 hali iliyopelekea kutokukubaliana na hilo.

Mara baada ya kusikiliza pande zote mbili, Mwenezi Makonda alibaini makosa ndani ya Ofisi ya Mkurugenzi na Kumtaka Mkuu wa Mkoa wa Manyara kwa mamlaka aliyonayo kutoa neno na ndipo akaagiza ndani ya siku 5 kulipwa kwa fedha hizo Tsh Milioni 27.5 kwa Vijana hao.

" *Tunawezaje kuwajengea Uchumi Vijana wa Nchi yetu kama iwapo hata kazi wanazofanaya kwenye Serikali yetu na bado hamuwalipi? Rais Samia anawapenda Vijana na kuwaamini kufanya hivi ni kumkosea na kuwanyima haki Vijana wetu* " Alisema Mwenezi Makonda.


📍 Mji mdogo wa Katesh


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG