BANDA MEDIA BLOG

MBOWE NI MNUFAIKA MKUBWA WA MARIDHIANO AMBAYO YAMEMFANYA AKAWA HURU NA KESI ZATE ZA KISIASA_ MAKONDA


"Kwa masikitiko makubwa jana tumepata nafasi ya kumsikia kaka yetu Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA akituhumu na kutoa kauli za kuzalilisha na kufedheesha na kutweza utu wa Kiongozi wetu bila kujali dhamira njema aliyoonyesha Mwenyekiti wetu wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ujenzi wa Umoja na Mshikamano katika Taifa letu"

"Taifa hili kwa mara ya kwanza limeshuhudia haki ikisimamiwa kikamilifu ikiwa pamoja na jitihada binafsi za Mwenyekiti wetu wa CCM na Rais wa Tanzania alizozifanya katika kuunda Tume ya Haki jinai kupitia mambo kadhaa wa kadhaa ili kuhakikisha kwamba Mtanzania anapata haki yake bila kujali rika, elimu kipato, kabila , dini na hata kule alipotokea"

"Mbowe kasema maneno mazito sana, upo wakati tumetafakari ya kwamba hakuna sababu ya kumjibu lakini imefika wakati tukasema Hapana...kwanini tumuache apotoshe umma kwa kichecheo ambacho hatuelewi msingi wake ni nini ?"

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG