MWANAFUNZI ATAKAYECHELEWA KURIPOTI SHULE KUKUMBANA NA ADHABU YA KULIMA MATUTA 10. RC SENYAMULE
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary
Senyamule ameyasema hayo 04, Januari 2024 wakati akiwa katika ziara
yake ya kikazi ya kukagua Miradi ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Michese na
kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma,
Kata ya Mkonze eneo la Michese.
Akizungumza na wananchi wa Michese
Mhe. Senyamule amesema mtoto atakaye chelewa kuanza Masomo kwa wakati atalima
matuta kumi.
“Wazazi msiwasababishie watoto adhabu ya kulima matuta kumi kwasababu ya kuchelewa kufika shule kwa wakati na kuchelewa kuanza masomo wanafunzi wanaanza kusoma tangu siku ya kwanza wanapofungua shule”
Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu wa Mkoa wa Dodoma Bw.Justin Machela amesema tuwapeleke watoto wetu shule na kuepuka Malalamiko yasiyo na Msingi ili kuhakikisha watoto wanaanza masomo kwa wakati na kuwanunulia vifaa vinavyoitajika Shuleni kama madaftari na kalamu.





