HIKI HAPA ENG HERSI ALICHOONGEA NA BOSI WAKE NA MBAPPE BAADA YA KUKUTANA NAE...
Rais wa Klabu ya Young Africans SC na Mwenyekiti wa Vilabu Barani
Afrika, Eng Hersi Said amekutana na Rais wa Klabu ya Paris Saint-Germain ya
Ufaransa na Mwenyekiti wa Vilabu Barani Ulaya, Ndugu Nasser Bin Ghanim
Al-Khelaifi, Jijini Paris Nchini Ufaransa, jana Januari 3, 2024.
Eng
Hersi alipewa mualiko maalum kutoka Kwa ndugu Nasser Bin Ghanim Al-Khelaifi kwa
lengo la kujadili jinsi vyama hivyo vikubwa vinavyoweza kujenga uhusiano mzuri
utakaosaidia maendeleo ya Vilabu Wanachama.
Habari
za YangaVilevile, Ndugu Nasser Bin Ghanim Al- Khelaifi alimkaribisha Eng Hersi
kushuhudia mchezo wa Fainali ya Trophée des Champions uliochezwa kwenye Uwanja
wa Parc de Prince, ambapo PSG ilibeba Ubingwa baada ya kuichapa Toulouse kwa
magoli 2-0
