Kuna kitu cha kipekee kuhusu ndege huyu ambaye mtaalamu wa ndege John Murillo alikiona katika Hifadhi ya Mazingira ya Don Miguel huko Colombia, karibu kilomita 10 kusini-magharibi mwa jiji la Manizales.
Ndege mwitu aliyevutia macho yake - anajuulikana kama Green Honeycreepers. Upande wake wa kushoto - manyoya ni ya rangi ya kijani kibichi, rangi ya ndege majike wa spishi hiyo, na upande wa kulia manyoya ni ya buluu, ndege madume.
"Inafurahisha sana. Wapenzi wengi wa ndege huishi maisha yao yote na hawaoni ndege mwenye jinsia mbili. Kwa hivyo ni bahati sana kufaidika na ugunduzi wa John," anasema mtaalamu wa wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Otago, New Zealand, Prof Hamish Spencer.
Anasema, ni nadra sana ndege kuwa namna hiyo. Na hajui mfano wa ndege kama huyo katika nchi yake ya New Zealand.
