Mjumbe wa mkutano Mkuu wa CCM, Asia Juma akifafanua jambo wakati alilipokuwa akifunga Mafunzo kwa wajasiriamali wa kata ya Nkuhungu, jijini Dodoma
Diwani wa Viti Maalum Jijini Dodoma Mary Nitwa akifurahia jambo wakati akizungumza na wajasiriamali wakata wa Nkuhungu muda mfupi kabla ya mafunzo hayo kufungwa.
Diwani wa Kata ya Nkuhungu Jijini Dodoma Daudi Mkandi, akisisitiza jambo wakati akizungumza na wajasiriamali hao.NA JOHN BANDA, DODOMA
WANAWAKE vijana
wametakiwa kujiepusha na vitendo vya ngono vinavyosababishwa na Mikopo ya
kausha Damu inayotolewa kwa masharti magumu ya Riba kubwa na Muda Mfupi.
Mikopo hiyo hutakiwa kurejeshwa kila siku 4,000 kwa kipindi cha siku 30 ambao ni mwezi mmoja kwa aliyekopa tsh 100,000, mkopaji anaposhindwa kurejesha siku moja hupigwa penati kwa siku inayofuata hutakiwa kulipa 12,000 pamoja na faini ya jana yake.
Diwani wa Viti maalum Jiji la Dodoma Mary Nitwa ametoa ushauri huo wakati wa Kufunga Mafunzo kwa wajasiriamali wa kata ya Nkuhungu yaliyofanyika kwa wiki moja yakiwajumuisha zaidi ya wakazi 200 wa kata hiyo bila Garama yoyote.
Diwani Nitwa Amesema kumekuwa na Tabia ya Baadhi ya vijana wa kike wanaojihusha na mikopo hiyo kujirahisha na vitendo vya ngono na wanaume kwa malengo ya kiulipiwa marejesho waliyokopa.
“wapo baadhi yenu na hapa najua mpo ambao mmekuwa mkikopa kwa kutegemea kwenda kujirahisha kwa wanaume mkiwalenga wawape fedha ili mkalipe Mikopo hiyo, nawaambia acheni hiyo ni tabia Mbaya”, amesema
Aidha amewataka washiriki
wote wa mafunzo hayo kwenda kuutumia ujuzi walioupata Kujiendeleza, kwa
kuanzisha Miradi badala ya kubaki wanakopa na kisha kuhamisha madeni kwa
wakopeshaji wengine
“yaani unakuta mtu anakopa pale kwa ajili ya kwenda kupeleka Rejesho la Mkopo mwingini, niwaambie tu naomba sana, mafunzo haya yawaondoe kwenye umasikini unawaowapekea kuwa kama watumwa, kuweni na jasili fanyeni biashara yako mkaheshimike”, amesema
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Taifa Aliyefika Kuyafunga Mafunzo hayo, Asia Juma amesema Chama chake kitaendelea kuunga mkono Juhudi hizo zinazofanywa na viongozi wa kata na mitaa kwa lengo la kuwaletea tija wananchi.
“hakikisheni bidhaa zebu mnazotengeneza zinakuwana kiwango bora kwa ajili ya kuingiza sokoni, kuhusu mikopo kuna mabenki hapa ambayo yamejinadi kuwa na asilimia 1 ni kama hakuna kabisa riba hivyo tukaicgangamkie”, amesema