BANDA MEDIA BLOG

ZAIDI YA ASILIMIA 88 YA WANAFUNZI MKOA WA DODOMA WAMERIPOTI SHULENI

 


Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Mwalimu 
Vicent Kayombo akifafanua jambo wakati alipoongea na waandishi wa habari ofisini kwake.
                     ............................................

NA JOHN BANDA , DODOMA

 ASILIMIA 88.88 ya wanafunzi walioandikishwa kujiunga  Darasa la Kwanza katika shule za Serikali mkoani Dodoma mpaka kufikia Januari 17, mwaka huu wameripotiwa kuanza masomo

 Akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Afsa Elimu Mkoa wa Dodoma Mwlalimu Vicent Kayombo amesema  Jumla ya wanafunzi 71,536 wamerioti shuleni kati ya wanafunzi 80,482 walioandikishwa na kutakiwa kujiunga na shule  ambapo amesema walioripoti  ni sawa na asilimia 88.88.  

 Kayombo Amesema kwa Upandewa wanafunzi waliojiunga na Kidato cha Kwanza wamefikia asilimia 57.31, kutoakana na walioripoti kufikia 30,306 ikilinganishwa na idadi ya 52,880 ambao  wamepangiwa kwenye shule serikali za mkoa wa Dodoma.

 Akiongelea wanafunzi waliojiunga madarasa ya Awali Kayombo Amesema mpaka kufikia Januari 17, mwaka huu waliokwisha Ripoti Shuleni ni 55.364 kati ya wanafunzi 65.471 walioandikishwa kujiunga na masomo katika mwaka huu mpya wa Elimu ambayo ni sawa na Asilimia 84.56

 AMBAO HAWAJAJIUNGA

Akizungumzia wanafunzi ambao bado awajajiunga na masomo mpaka sasa Afisa Elimu Huyo amesema kumekuwa juhudi kubwa za kuhamasisha wazazi ili wawepeleke shule watoto wao zinazofanywa na Serikali ya Mkoa.

 “Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule  amekuwa akitoa maelekezo kuwa wanafunzi wote walioandikishwa na  waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza, wapelekwe shule na wazazi wao kwa muda ulipangwa na kama hawana sare za shule wapewe madaftari na kalamu wakaanze masomo, vifaa vingine vya shule vitawakuta masomoni”. amesema

 Sambamba na hayo Mwl. Kayombo ametoa rai kwa wazazi na walezi  kuhakikisha watoto wao wana hudhuria shuleni kila siku tangu siku anayoanza shule na kuendelea kusimamia mahudhurio na maendeleo ya watoto wao mashuleni.


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG