RAIS DK. SAMIA ATAJA MAFANIKIO LUKUKI 2023, ATIRIRIKA MIPANGO KAMAMBE 2024, NI KATIKA HOTUBA YAKE KUAGA 2023 NA KUULAKI 2024
Rais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ameainisha mipango ya serikali
kwa mwaka mpya wa 2024, ikiwemo agizo la kuanzisha safari za SGR kati ya Dar es
Salaam na Dodoma, na kuanza kazi kwa bwawa la umeme la Julius Nyerere.
Katika hotuba yake ya kuuaga mwaka wa 2023 na kuukaribisha 2024, Rais Dk. Samia
ametaja masuala makuu yaliopewa umuhimu katika mwaka wa 2023 huku akielezea
mipango ya serikali katika mwaka huu mpya.
Hotuba yake ilijikita katika masuala makuu 12 kuanzia amani na usalama, sera za
kiuchumi hadi mabadiliko ya tabianchi.
Rais Samia amesema imani ya wawekezaji kwa Tanzania imeongezeka katika mwaka
unaomalizika ambapo miradi 55 kati ya 504 iliyosajiliwa na kituo cha uwekezaji,
TIC, ilikuwa ya upanuzi wa uwekezaji uliopo tayari, huku makusanyo ya kodi
yakiongezeka kwa asilimia 8 hadi shilingi trilioni 22.6 ikilingnisha na mwaka
2022.
"Hivyo, jinsi uchumi wetu unavyokua, tutaendelea kuongeza makusanyo
kupitia mifumo madhubuti ya ukusanyaji na kuhakikisha kodi inakusanywa kwa
uadilifu na kwa kuzingatia sheria," alisema Rais Samia.
Sekta za uzalishaji zinazo jumuisha kilimo, madini na utalii, ambazo ndio
tegemeo la uchumi, zimeendelea kuwekewa msisitizo, "ili kuwafikia
wazalishaji wengi zaidi, hususan wale wadogo na kuchochea uzalishaji kuanzia
ngazi za chini," alisema Rais Samia, na kuongeza kuwa wameongeza bajeti ya
kilimo kutoka shilingi bilioni 751 mwaka jana 2022 hadi sh. bilioni 970 mwaka
uliomalizika, ongezeko sawa na asilimia 29.
"Uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kutoka tani 17,148,290 msimu
wa 2021/2022 hadi tani 20,402,014 msimu wa mwaka 2022/2023, hivyo
kufikisha asilimia 124 ya kiwango cha utoshelevu wa chakula nchini,"
alisema Rais huyo mwanamke wa kwanza kuiongoza Tanzania. "Vilevile,
tumehakikisha mazao makuu yanauzwa kwa njia ya minada ili kupata bei nzuri , na
tumeanzisha mnada mpya wa
zao la chai."
Kuongeza ushiriki wa vijana na wanawake katika kilimo
Rais Samia amesema serikali imeendelea na juhudi za kuwashirikisha vijana na wanawake
katika kilimo ambapo jumla ya ekari 201,241 zimetengwa kwa shughuli hiyo.
Katika kuimarisha juhudi hizo, Rais Samia amesema serikali yake
imeanzisha programu ya kilimo cha kisasa iitwayo Jenga Kesho Iliyo Bora
(BBT) ili kuongeza uzalishaji, kuchochea viwanda vya usindikaji, na kutengeneza
ajira kwa vijana.
Katika kutambua mchango mkubwa wa wachimbaji wadogo kwenye sekta hii mwaka huu,
Samia amesema serikali ilinunua mitambo mitano ya uchorongaji kwa ajili ya
wachimbaji hao ili kuongeza tija zaidi na mchango wao kwenye sekta ya madini.
"Mwelekeo wa serikali ni ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani ya madini
hapa nchini, hatua itakayotuwezesha kuongeza thamani na fursa zaidi za
ajira," alisema Rais katika hotuba hiyo iliyotangazwa moja kwa kupitia
kupitia televisheni.
Pia Rais Samia alizungumzia hatua zilizochukuliwa kuimarisha sekta ya utalii
ambayo imechangia kiasi cha dola ma Marekani bilioni 3.22 kufikia Oktoba 2023
ikilinganishwa na dola za Kimarekani Bilioni 2.33 kipindi kama hicho mwaka 2022.
"Manufaa haya yametokana na juhudi za Serikali na wadau wa sekta hii.
Hivyo, n itoe rai kwa watoa huduma kwenye sekta ya utalii , ku endele a
kuimarisha huduma zao, na kwa Watanzania wa naoishi maeneo ya vivutio,
tuendelee kudumisha ukarimu kwa wageni ili tuendelee kupokea watalii wengi
zaidi."
Maendeleo ya sekta ya
usafiri
Rais Samia ametoa agizo kwa mamlaka ya usafiri wa reli nchini Tanzania,
kuhakikisha kwamba ifikapo mwisho wa Julai 2024, huduma za usafiri kupitia njia
ya kisasa ya SGR ziwe zimeanza. "Wananchi wamechoshwa na vijisababu,
wanataka kuona reli ikifanya kazi," alisema Rais.
Rais Samia alisema serikali imeendelea kuwekeza katika unenzi wa moindombinu ya
barabara, madaraja na vivuko katika mikoa mbalimbali ya nchi, na kufahamisha
kuwa ujenzi wa SGR kutoka Dar es Salaa, hadi Morogoro na kutoka Morogoro hadi
Makutupora umekamilika kwa asilimia 90.
Aidha, mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika, utawezesha ujenzi wa kipande
cha Tabora hadi Kigoma na Uvinza hadi Musongati.
Kwenye usafiri wa majini, Rais amesema serikali imekamilisha ujenzi wa gati
katika bandari mpya ya Karema kwenye Ziwa Tanganyika, inayotazamiwa kufungua
uchumi, biashara, na muingiliano wa watu na DRC na hivyo kukuza uchumi wa Mikoa
ya Kigoma, Rukwa na Katavi.
Kwa upande wa usafiri wa anga, Rais Samia amesema serikali ilikamilisha ununuzi
wa ndege moja ya mizigo na moja ya abiria, huku mashirika mbalimbali ya ndege
ya kimataifa kama vile Air France na Saudi Airlines yakivutiwa kuanza kutoa
huduma za safari kwenda Tanzania. "Tunaamini uwekezaji huu utaimarisha
sekta ya utalii na utakuza pia biashara ya kilimo cha maua na mbogamboga."
Kuanza kazi kwa bwawa la umeme la Nyerere Rais Samia amekiri juu ya changamoto
ya mgao wa umeme ambao umegeuka sugu na kuathiri ukuaji wa uchumi wa taifa hilo
la Afrika Mashariki. Amesema tatizo hilo ndiyo liliifanya serikali kuchukua
uamuzi mwaka 2017 kuanzisha mradi za bwawa la umeme la Julius Nyerere, ambalo
linatazamia kuingiza megawati 2,115 kwenyw gridi ya taifa.
Rais amefahamisha kuwa mwezi Februari mtambo wa kwanza wa kuzalisha umeme
bwawani hapo utawashwa rasmi, na mtambo wa pili utawashwa mnamo mwezi Machi.
Mitambo hiyo miwili itazalisha jumla ya megawati 470 na hivyo kufidia upungufu
wa sasa ambao ni megawati 300.
"Ni imani yangu na Serikali kwa ujumla kuwa, hatua hizi zita leta ufumbuzi
w a kudumu kwa suala la mgao wa umeme nchini," alisema Rais Samia na
kuongeza kuwa serikali inaendelea pia kuwekeza kwenye vyanzo vingine vya umeme
kama vile gesi, jua, na upepo , ili kuongeza upatikanaji wa uhakika wa nishati
hiyo.
Uwekezaji kwenye sekta ya
afya.
Rais Samia amesema nguvu kubwa imewekwa kwenye kuimarisha huduma za afya kwa
kuajiri wataalam, ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitendea kazi. Amesema mwaka
2023, serikali imeajiri jumla ya wataalam 17,309 na ilitenga jumla ya shilingi
bilioni 190.9 kwa ajili ya kununua dawa.
Rais amesema uwekezaji unaofanywa wenye sekta ya afya umeleta matokeo
yanayoonekana dhahiri, ambapo kuanzia mwezi Januari mpaka Novemba, 2023, jumla
ya wananchi 15,386 wamepata huduma za CT Scan kwenye Hospitali za Rufaa za
Mikoa nchini kote na hii imesaidia katika kuimarisha mfumo wa rufaa na huduma
za uchunguzi kwa Mikoa yote.
Jumla ya wagonjwa 200 wamepimwa kipimo cha MRI katika hospitali za rufaa za
kanda ya Mbeya, Chato, na Mtwara. "Hospitali hizi hazikuwahi kuwa na
kipimo cha aina hii, hivyo uwepo wa mashine za MRI zimeleta ahueni ya gharama
kwa wananchi wa kanda husika," alisema rais.
Elimu, Diplomasia na
Tabianchi
Rais pia amezungumzia juhudi za kuboresha sera na mitaala ya elimu,
kushughulikia changamoto za malazi ya walimu, na kuongeza bajeti ya mikopo ya
wanafunzi.
Kuhusu mahusiano ya kimataifa, Rais Samia ameelezea mafanikio katika mazungumzo
ya kidiplomasia, kupata misaada ya kifedha, kuunda fursa za bidhaa za
Kitanzania katika masoko ya kimataifa, na kurejea katika programu za maendeleo
kimataifa.
Ametaja fursa za Tanzania kuwakilishwa katika mikutano muhimu ya kimataifa kama
vile wa mataifa ya kundi la BRICS, Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya
Afrika, Jukwaa la Uchumi la Davos na mikutano ya Afrika na nchi mbali mbali
zenye nguvu za kiuchumi.
Ametaja pia wageni kadhaa mashuhuri walioitembelea Tanzania, wakiwemo Makamu wa
Rais wa Marekani Kamala Harris, Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier,
Marais wa Indonesia, Hungary na Romasia pamoja na nchi jirani na rafiki za
Afrika. Pia ametaja ziara alizozifanya nje ya nchi na kuorodhesha mafanilioni
yaliotokana na ziara hizo.
Amehimiza uhifadhi wa mazingira, na kushughulikia changamoto zinazosababishwa
na matukio ya hali ya hewa yanayohusiana na El Nino, na kuwataka wananchi
waendelee na juhudi za kupanda miti milioni 1.5 kila mwaka kama inavyoeleza
ilani ya chama tawala, Chama cha Mapinduzi, CCM.
